Vulogu (kwa Kiingereza: vlog) ni aina ya blogu ambayo huwa mbinu yake ya uwasilishaji wa jumbe ni kwa kutumia video.
Kwa mapana, vulogu ni blogu ya video (video blog). Kwa wengi, video zao huwekwa kwa wavuti ya Youtube ambayo ndiyo iliyo na video nyingi sana.
Msanii Nelson Sullivan alijulikana kwa kurekodi kazi yake na kuiwasilisha kwa watu kwa kutumia vulogu. Kazi yake aliiweza kurekodi katika miji tofauti kama vile New York.
Vulogu zilipata umaarufu sana mwaka 2005. Leo, ni watu wengi walio na vulogu zinazowasilisha jumbe tofauti kutoka masomo ya kupika, hisabati, uchumi, malezi, urembo na hata afya njema ya mwili.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Vulogu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.