Uvimbe wa ubongo (kwa Kiingereza encephalitis) ni ugonjwa ambao husababisha ubongo kuvimba ghafla.
Kwa kawaida husababishwa na virusi, bakteria (kwa Kiingereza Granulomatous amoebic encephalitis), au vijidudu vingine. Kadiri ubongo unavyovimba, huweza kuharibiwa wakati unapokwaruzana na fuvu.
Uvimbe wa ubongo unaweza kusababisha dalili hatarishi kama vile kupata kifafa na kiharusi, na hii inaweza kuwa mbaya zaidi.
Mwaka 2013, ugonjwa wa uvimbe wa ubongo uliua watu 77,000 duniani.
Kwa kawaida, watu wazima wenye ugonjwa wa uvimbe wa ubongo wana homa inayoanza ghafla, maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, na wakati mwingine kifafa. Watoto wadogo au watoto wachanga wanaweza kuwa na hasira, hawataki kula, na hupatwa na homa.
Kwa kawaida wagonjwa huwa wanachoka sana au wanachanganyikiwa.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uvimbe wa ubongo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Uvimbe wa ubongo, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.