Maria Alphonsa Muttathupadathu (Kudamalloor, karibu na Kottayam, huko Kerala19 Agosti 1910 - Bharananganam, 28 Julai 1946) alikuwa bikira Mfransisko wa Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar nchini India.
Ili asiolewe kwa shuruti, alijichoma mguu kwa kuuweka motoni. Kisha kupokewa katika shirika ya Waklara wa Kimalabari, alimtolea Mungu maisha yake yote akiwa mgonjwa karibu mfululizo.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Yohane Paulo II tarehe 8 Februari 1986 akatangazwa mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 12 Oktoba 2008.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Maria Alfonsa Matathupadathu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.