Kige'ez (kwa maandishi ya Kiamhari: ግዕዝ; matamshi: gē-ĕz) ni lugha ya kale ya Ethiopia iliyozungumzwa zamani za ufalme wa Aksum.
Baadaye ilikuwa lugha ya kimaandishi nchini Ethiopia hadi karne ya 19 na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la orthodoksi la Ethiopia.
Huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti za kusini. Hutazamiwa kama lugha mama ya lugha za kisasa kama Kiamhari na Kitigrinya na Kitigre nchini Ethiopia na Eritrea.
Maandishi ya Kige'ez ni aina ya abugida yenye herufi 26 za konsonanti na 4 za vokali zinazounganishwa kuwa alama 202 kwa silabi zote zinazowezekana. Mifano ya kwanza inyojulikana ni kutoka karne ya 4 BK.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kige'ez, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.