Kapteni ni cheo cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia.
Kapteni huwa ni kiongozi wa kikosi cha askari 100-200.
Madaraka ya kapteni ni kuongoza kikosi chake akisaidiwa na maluteni wake. Kwa kawaida hatashiriki katika mipango ya vita bali wajibu wake ni kutekeleza maagizo ya wakubwa wake.
Katika jeshi la wanamaji kapteni (captain) hutokea kama cheo cha kiongozi wa manowari kwa hiyo kuna uwezekano ya kwamba kapteni huyu ana madaraka zaidi kuliko kapteni kwenye nchi kavu.
Neno limeingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Asili ya cheo ni neno la Kilatini "caput" linalomaanisha "kichwa, mkubwa, kiongozi wa kundi".
Vyeo vya kijeshi - Tanzania | ||
---|---|---|
Jenerali * Luteni Jenerali * Meja Jenerali * Brigedia * Kanali * Luteni Kanali * Meja * Kapteni * Luteni * Luteni-usu Afisa Mteule Daraja la Kwanza * Afisa Mteule Daraja la Pili * Sajinitaji * Sajenti * Koplo * Koplo-usu |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kapteni, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.