Kaisari Wilhelm Ii

Kaisari Wilhelm II (jina kamili: Friedrich Wilhelm Viktor Albert von Hohenzollern; 27 Januari 1859 – 4 Juni 1941) alikuwa mfalme wa mwisho wa Prussia na kaisari wa mwisho wa Ujerumani kuanzia mwaka 1888 hadi 1918.

Kaisari Wilhelm Ii
Wilhelm II
Kaisari Wilhelm Ii
Wilhelm II kwenye rupia ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Maisha

Alizaliwa na mfalme mteule Friedrich III akiwa mjukuu wa Kaisari Wilhelm I. Baba yake alikufa baada ya utawala mfupi wa siku 99 pekee, hivyo Wilhelm II akawa mfalme na kaisari akiwa na umri wa miaka 29. Mwanzoni alitawala pamoja na chansella Otto von Bismarck lakini baada ya miezi michache alifarakana naye na kumwachisha.

Wilhelm alitaka kupatanisha wafanyakazi wa Ujerumani -waliofuata chama cha kisoshalisti- na utawala wa kifalme lakini hakuwa tayari kuongeza demokrasia. Alichukia bunge lililokataa mara kadhaa madai yake ya kupanua jeshi. Alipigania upanuzi wa jeshi la maji, uliojenga wasiwasi wa Uingereza juu ya uhusiano wake na Ujerumani.

Akiwa pia mkuu wa makoloni ya Ujerumani, kama vile Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Aliona koloni kama suala la heshima ya kitaifa, ilhali hakujali wenyeji na tamaduni zao.

Wataalamu wanaona ya kwamba alikuwa na jukumu kubwa kwa kutokea kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Mwaka 1918, baada ya vita ya miaka minne, wafanyakazi na wanajeshi wa Ujerumani waligoma. Wilhelm pamoja na wafalme na makabaila wote wa Ujerumani walipinduliwa hata Ujerumani ilipata kuwa jamhuri. Wilhelm alihamia Uholanzi alipoishi hadi mwaka 1941. Hapo alikufa na kuzikwa kwa sababu hakutaka kuzikwa katika Ujerumani isiyo na utaratibu wa kifalme.

Viungo vya nje

Kaisari Wilhelm Ii 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

185918881918194127 Januari4 JuniKaisariMfalmeMwakaPrussiaUjerumani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WagogoSarufiFananiUkristoMlima wa MezaFani (fasihi)IsimuJacob StephenUtumwaVivumishi vya pekeeKukiMoscowHadhiraBendera ya KenyaCleopa David MsuyaKiingerezaWizara za Serikali ya TanzaniaRupiaChristopher MtikilaYesuHisiaMichezoWimboUkutaKoloniUsawa (hisabati)DuniaRaiaMungu ibariki AfrikaUtumbo mpanaBawasiriDawatiMandhariMkoa wa KilimanjaroUchaguziJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaRicardo KakaJoseph ButikuTume ya Taifa ya UchaguziP. FunkKiambishi awaliHektariMaandishiChumba cha Mtoano (2010)Barua pepeKigoma-UjijiMkoa wa MaraNgono zembeUbadilishaji msimboOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMawasilianoMeno ya plastiki25 ApriliNomino za jumlaIsraeli ya KaleMkanda wa jeshiMkwawaKabilaNyotaMkoa wa ManyaraBungePesaMkoa wa MbeyaUlumbiMzeituniUshairiHali ya hewaMnyamaHistoria ya uandishi wa QuraniZabibuUharibifu wa mazingiraMkoa wa SongweShukuru Kawambwa🡆 More