Kaharabu

Kaharabu (kutoka Kiajemi کهربا kahroba; kwa Kiingereza amber) ni rezini (si utomvu) ya kisukuku cha miti iliyokua miaka milioni iliyopita.

Inaweza kufanana na aina za sandarusi lakini kwa jumla umri wake ni mkubwa na ni mgumu zaidi kuliko sandarusi. Aina bora za kaharabu zinajulikana pia kwa jina la kitaalamu la succinit.

Kaharabu
Mapambo ya vito vya kaharabu
Kaharabu
Rezini ya ubao wa miti ni chanzo cha kaharabu

Matumizi yake ni hasa kwa mapambo, kama kito, lakini pia kama sehemu ya dawa la mitishamba.

Kaharabu inatokea katika sehemu nyingi za dunia; kiwango kikubwa kabisa duniani (hadi sasa 90%) kimepatikana kutoka pwani za Bahari Baltiki, hasa eneo la Samland

Kaharabu ilitokea katika mazingira ya misitu ya miti yenye rezini husika iliyoendelea kuwa kisukuku katika mchakato wa kufunikwa na maganda manene ya udongo yaliyosababisha shinikizo la tani nyingi na joto kwa miaka elfu na zaidi.

Matumizi na biashara ya kaharabi inajulikana kutokana na utafiti wa kiakiolojia tangu miaka 12,000 hivi. Wagiriki wa Kale waliita kaharaba kwa jina "elektron" wakatambua ya kwamba kipande cha kaharaba baada ya kusuguliwa kinavuta sehemu ndogo za kitambaa au nyuzi kwake. Hapa ni asili ya neno "electric" (umeme) katika lugha za Ulaya.

Kaharabu
Mbu wa kale katika kipande cha kaharabu.

Katika elimu ya historia ya viumbehai kaharabu ni muhimu kwa sababu mara nyingi vipande vyake vinatunza wadudu na viumbe wengine wadogo waliokaa kwenye miti na kufunikwa ndani ya kitone cha rezini bichi. Wadudu hao wamehifadhiwa hivyo kwa miaka milioni kadhaa na leo wanapatikana kwa uchunguzi wa kitaalamu.

Marejeo

Tags:

JinaKiajemiKiingerezaKisukukuMilioniMitiUmriUtomvu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

LahajaMikoa ya TanzaniaUongoziTanganyika (maana)Kiwakilishi nafsiTulia AcksonMkuu wa wilayaWahadzabeLuhaga Joelson MpinaMwanzo (Biblia)Ngono zembeMaajabu ya duniaVitenzi vishiriki vipungufuYesuMadiniPasakaUjimaShukuru KawambwaJumuiya ya Afrika MasharikiMuhimbiliUzazi wa mpango kwa njia asiliaVivumishi vya urejeshiAmri KumiKitenzi kikuuMwanza (mji)Orodha ya milima mirefu dunianiJumuiya ya MadolaNominoMartin LutherMatiniFasihi andishiUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaBungeOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaFasihi simuliziMafumbo (semi)Nembo ya TanzaniaMoyoMaana ya maishaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniOrodha ya makabila ya TanzaniaKonyagiJuxHafidh AmeirBiasharaNg'ombe (kundinyota)DivaiHomoniNahauUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Bonde la Ufa la Afrika ya MasharikiSwalaPasifikiMkoa wa DodomaMalariaKiarabuTanzaniaKisukuruMfuko wa Taifa wa Hifadhi ya JamiiNgw'anamalundiNomino za wingiDaktariMkoa wa TaboraGongolambotoUpepoMziziEthiopiaMoses KulolaViwakilishi vya kumilikiBendera ya TanzaniaJinaAfrika KusiniSimba🡆 More