Homa Ya Rumatizimu

Homa ya rumatizimu (kwa Kiingereza: rheumatic fever; kifupi chake: ARF yaani homa kali ya rumatizimu) ni ugonjwa wa kuvimba unaoweza kuhusisha moyo, jointi, ngozi, na ubongo.

Ugonjwa huu hujijenga majuma mawili hadi manne baada ya maambukizi ya koo.

Homa ya rumatizimu
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyCardiology Edit this on Wikidata
ICD-10I00.-I02.
ICD-9390392
DiseasesDB11487
MedlinePlus003940
eMedicinemed/3435 med/2922 emerg/509 ped/2006
MeSHD012213

Ishara na dalili ni joto jingi, maumivu mengi ya jointi, kwenenda kusikohiari kwa misuli, na vipele visivyo vya kawaida visivyowasha vijulikanavyo kama erythema marginatum. Moyo huhusika katika takribani nusu ya visa. Uharibifu wa kudumu wa vali za moyo, ujulikanao kama ugonjwa wa rumatizimu wa moyo (RHD), hutokea baada ya mashambulio mengi lakini huenda ukatokea mara kwa mara baada ya kisa kimoja cha ARF. Vali zilizoharibiwa zinaweza kusababisha mshtuko wa moyo. Vali hizo zisizo za kawaida pia huongeza hatari ya mtu huyo kupata fibrilesheni ya atriamu na maambukizi ya vali za moyo.

Kisababishi

Homa kali ya rumatizimu inaweza kutokea kufuatia maambukizi ya koo kwa bakteria iitwayo Streptococcus pyogenes. Isipotibiwa ARF hutokea kwa hadi asilimia tatu ya watu. Mwenendo halisi unaaminiwa kuwa utoaji wa antibodi dhidi ya tishu za mtu huyo. Watu wengine kutokana na jenetikia yao wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo kuliko wengine wanapotangamana na bakteria hiyo. Visababishi vingine vya hatari ni utapiamlo na umaskini.

Utambuzi wa ARF hutegemea kuwepo kwa ishara na dalili pamoja na thibitisho la kuwepo kwa maambukizi ya streptokokasi hivi karibuni.

Kinga na tiba

Kutibu watu walio na maumivu ya koo kwa antibiotiki, kama vile penicillin, hupunguza hatari yao ya kupata homa kali ya rumatizimu. Hii huhusisha kupima watu walio na koo zenye maumivu kwa maambukizi, kipimo ambacho huenda kisipatikane katika nchi zinazostawi. Mbinu zingine za uzuiaji ni usafi bora.

Kwa walio na ARF na RHD vipindi virefu vya antibiotiki vimependekezwa wakati mwingine. Urejeleaji wa polepole wa shughuli za kawaida unaweza kufanyika kufuatia shambulio. Baada ya RHD kujijenga, matibabu ni magumu zaidi. Mara kwa mara upasuaji wa kubadilisha vali au kukarabati huhitajika. Vinginevyo matatizo hutibiwa namna ya kawaida.

Epidemiolojia

Homa kali ya rumatizimu hutokea kwa takribani watoto 325,000 kila mwaka na takribani watu milioni 18; sasa hivi wana ugonjwa wa rumatizimu wa moyo. Wanaopata homa kali ya rumatizimu mara nyingi huwa na umri wa kati ya miaka 5 na 14, huku asilimia 20 ya mashambulio ya mara ya kwanza ikitokea kwa watu wazima. Ugonjwa huu hupatikana sana katika nchi zinazostawi na katika wazawa wa nchi zilizostawi.

Katika mwaka wa 2013 ulisababisha vifo 275,000, idadi iliyo chini kuliko vifo 374,000 katika mwaka wa 1990. Vifo vingi hutokea katika nchi zinazostawi ambako takribani asilimia 12.5 ya watu walioambukizwa wanaweza kufariki kila mwaka.

Maelezo ya ugonjwa huu yanaaminiwa kuanza angalau katika karne ya 5 katika maandishi ya Hippocrates. Ugonjwa huo ulipewa jina hilo kwa sababu dalili zake zinafanana na zile za baadhi ya magonjwa ya rumatizimu.

Marejeo

Homa Ya Rumatizimu  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homa ya rumatizimu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Homa Ya Rumatizimu KisababishiHoma Ya Rumatizimu Kinga na tibaHoma Ya Rumatizimu EpidemiolojiaHoma Ya Rumatizimu MarejeoHoma Ya RumatizimuJumaKifupiKiingerezaMaambukiziMoyoNgoziUbongoUgonjwa

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Simba (kundinyota)WaheheMziziMajina ya Yesu katika Agano JipyaNdovuMartin LutherMaktabaArusha (mji)HaitiNgeliCleopa David MsuyaMwanaumeKhalifaHisiaKaswendeMasafa ya mawimbiRitifaaKiarabuKiswahiliKichochoTulia AcksonMikoa ya TanzaniaUhifadhi wa fasihi simuliziSabatoMsamiatiMatumizi ya LughaIdi AminUkristo nchini TanzaniaUkooEthiopiaNyukiMzabibuMkoa wa MorogoroUtumwaBikiraWilaya ya UbungoMnururishoMbuga za Taifa la TanzaniaStashahadaMaudhui katika kazi ya kifasihiVipera vya semiKoloniNg'ombeWakingaUtumbo mwembambaMobutu Sese SekoRita wa CasciaPijiniMbaraka MwinsheheMtandao wa kompyutaTafakuriTabataMsokoto wa watoto wachangaUenezi wa KiswahiliSamakiAsili ya KiswahiliUmoja wa MataifaIkwetaWilaya ya TemekeWikipediaUfahamuOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKifaruKimara (Ubungo)Israeli ya KaleMkoa wa Unguja Mjini Magharibi25 ApriliHistoria ya TanzaniaTungoTetekuwanga🡆 More