Falsafa ya Kiafrika inaweza kumaanisha falsafa ya wasomi Waafrika, au falsafa inayopendekeza mtazamo wa Waafrika, au falsafa inayotumia mbinu maalumu za Kiafrika.
Kabla ya Uzodinma Nwala kuanza kufundisha somo hilo, hakukuwa na chuo kikuu chochote kilicholifundisha.
Falsafa ya Kiafrika inaweza kufafanuliwa kama hoja za Waafrika juu ya mang'amuzi ya maisha yao.
Hiyo ilikuwepo hata kabla ya ukoloni uliowakutanisha na falsafa ya Magharibi.
Hasa Misri ya Kale iliwahi sana kuwa na falsafa yenye utajiri wa mawazo, halafu ikachangia falsafa ya Kigiriki na falsafa ya Kikristo.
Katika karne ya 20 tapo la kupinga ukoloni Afrika lilichochea hasa falsafa ya kisiasa ambayo ilipata maitikio makubwa ndani na nje ya bara hilo, ikichochea juhudi za ukombozi sehemu nyingi. Mfano mmojawapo ni falsafa ya Ujamaa iliyozaliwa na Julius Nyerere nchini Tanzania.
|
|
|
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Falsafa ya Kiafrika, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.