Milima Atlas

Kwa matumizi tofauti ya jina hili tazama Atlas (maana)

Milima Atlas
milima ya atlas
Milima Atlas
Safu za milima ya Atlas.

Milima ya Atlas (kwa Kiberber: Idurar n Watlas; kwa Kiarabu: جبال الأطلس‎, jibaal al-atlas) ni safu ya milima kunjamano katika Afrika ya kaskazini-magharibi. Ina urefu wa takriban kilomita 2,400 kuanzia Moroko kwa kuvukia Algeria hadi Tunisia. Milima ya Atlas hutenganisha pwani ya Atlantiki na Mediteranea kutoka jangwa la Sahara.

Mwinuko wa juu ni Jebel Toubkal nchini Moroko inayofikia mita 4,167 juu ya UB.

Wakazi wa milima hii ni hasa makabila ya Waberber.

Jina la milima hii linatokana na mmoja wa miungu ya Ugiriki ya Kale, Atlas.

Asili

Atlas ni milima kunjamano yaani tokeo la kugongana kwa mabamba ya gandunia ya Afrika na Ulaya kulikosababisha kukunjwa kwa uso wa ardhi na kutokea kwa safu za milima hii. Mchakato huu ulitokea mara mbili. Mara ya kwanza takriban miaka milioni 300 iliyopita, wakati bamba la Amerika Kaskazini liligongana na bamba la Afrika na tokeo lake ni safu ya Antiatlas katika Moroko ya kusini. Lakini sehemu kubwa ya Atlas ilitokea kutokana na mgongano wa mabamba ya Afrika na Ulaya katika kipindi cha miaka milioni 65 - 2 iliyopita.

Kutokana na historia hii kuna hatari ya mtetemeko wa ardhi katika eneo la Atlas na miji kadhaa iliwahi kuharibiwa.

Jina

Jina la Atlas linatokana na mhusika Atlas kwenye mitholojia ya Ugiriki ya Kale. Katika hadithi za Wagiriki huyu alikuwa mungu mmojawapo aliyepaswa kubeba anga kwa mabega yake. Hivyo makazi yake yaliaminiwa kuwa katika milima hiyo mirefu iliyo karibu na anga.

Tazama pia

Marejeo

Milima Atlas  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Atlas (milima) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Milima Atlas AsiliMilima Atlas JinaMilima Atlas Tazama piaMilima Atlas MarejeoMilima AtlasAtlas (maana)

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Usultani wa ZanzibarSalaKadhiVidonda vya tumboKilimanjaro (volkeno)Tendo la ndoaJohn MagufuliJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaKen WaliboraNg'ombeMnara wa BabeliKanadaParachichiUharibifu wa mazingiraUzazi wa mpangoGeorDavieMkoa wa IringaEthiopiaOrodha ya wanamuziki wa AfrikaTabianchi ya TanzaniaVichekeshoJumba la MakumbushoDiraUaVihisishiHoma ya mafuaSadakaPesaBikiraMkoa wa TaboraUhindiMkoa wa ManyaraRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniSexAli KibaUkweliUenezi wa KiswahiliOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoMungu ibariki AfrikaMagonjwa ya kukuIsha RamadhaniMwaka wa KanisaMdalasiniMkoa wa MtwaraShetaniSamakiMatiniMzabibuKampuni ya Huduma za MeliMkoa wa Unguja Mjini MagharibiOrodha ya Marais wa NamibiaSemiNominoRushwaKipindupinduMfumo wa JuaKitenzi kikuuOrodha ya nchi za AfrikaVita ya Maji MajiVielezi vya idadiDubai (mji)TabainiOrodha ya Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoKifaruDiniWaluoUislamu nchini São Tomé na PríncipePijini na krioliAzam F.C.Nguzo tano za UislamuTetekuwangaOrodha ya Marais wa Marekani🡆 More