Adam Smith (16 Juni, 1723 - 17 Julai, 1790) alikuwa mwanafalsafa nchini Uskoti aliyeweka misingi kwa Sayansi ya Uchumi ya isasa.
Katika kitabu chake "Uchunguzi juu ya utajiri wa mataifa" (An Inquiry into the Nature and Causes of the Wealth of Nations) alieleza ya kwamba kama kila mtu ana nafasi ya kufuatilia faida yake ya binafsi ni afadhali kwa maendeleo ya taifa lote. Aliona njia hii kuwa afadhali kuliko serikali kupanga mambo ya uchumi kwa sababu kila mtu anajua mwenyewe mahitaji na uwezo wake. Aliona ya kwamba
Aliona ya kwamba msingi wa uchumi ni kazi ya watu inayoongeza thamani ya maliasili na arhi yenyewe. Kila mtu ana uwezo wa pekee na nafasi za pekee hivyo watu wanaelekea kuchagua sehemu ya nafasi zilizopo. Hii ni msingi wa ugawaji wa kazi mbalimbali kati ya watu. Nafasi ya kubadilishana mazao ya kazi kwenye soko huria inaleta matokeo bora kwa watu wote.
Nadharia hii imekuwa msingi wa falsafa ya ubepari lakini pia Karl Marx alitumia matokeo ya utafiti wa Smith kwa nadharia zake za usoshalisti.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Adam Smith, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.