Trigonometria (kutoka Kigiriki trigonon = pembetatu na metron = kipimo, upimaji) ni sehemu ya jiometria, hivyo ni tawi la hisabati.
Inatazama habari za pembetatu na uhusiano kati ya pande na pembe. Uhusiano kati ya urefu wa pande na ukubwa wa pembe hufuata kanuni fulani na kwa kujua kanuni hizo inawezekana kukadiria umbali wa kitu au ukubwa la eneo kwa kujua habari chache tu.
Elimu hiyo ilitokea wakati wa utamaduni wa Ugiriki ya Kale wakati wataalamu walifanya utafiti wa nyota na kukadiria umbali wa nyota na dunia. Walitambua kanuni za trigonometria kwa mfano wa pembetatu mraba. Ilhali kila pembetatu inaweza kugawiwa kwa pembetatu mraba mbili, elimu hiyo inatosha kujibu maswali mengi.
Kwa kawaida trigonometria inatazama maumbo bapa lakini kuna pia trigonometria ya tufe, yaani kuangalia pembetatu zilizopo usoni wa tufe au mpira.
Trigonometria inafuata hasa kanuni za pembetatu mraba, yaani pembetatu ambako pembe moja ina nyuzi 90°.
Jumla ya pembe 3 za pembetatu daima ni nyuzi 180°. Kwa hiyo kama pembe moja ni pembemraba (=90°) zile mbili nyingine ni pembe kali ambazo kwa jumla zina pia nyuzi 90 maana ni vikamilisho pembemraba.
Kwa hiyo kama pembe moja ya pembetatu ina nyuzi 90° na moja nyingine kati ya pembe tatu inajulikana basi hata ukubwa wa pembe ya tatu si siri tena.
Mara viwango vya pembe vinapojulikana tunaweza pia kujua uhusiano wa urefu baina ya pande. Kwa hiyo kama urefu wa upande mmoja unajulikana inawezekana kutaja urefu wa pande nyingine pia.
Majina yafuatayo hutumiwa katika trigonometria kwenye pembetatu mraba:
Kuna fomula husisho (ing. functions) tatu kwa pembetatu mraba katika trigonometria. Pamoja na husisho kinyume (ing. "reciprocals") kuna sita kwa jumla.
Sini (ing. sine, sinus, kifupi sin) - Sini ya pembe ni sawa na
Kosini (ing. cosine, cosinus, kifupi cos) - Kosine ya pembe ni sawa na
Tanjenti (ing. tangent, kifupi tan) - Tanjenti ya pembe ni sawa na
Husisho kinyume za husisho hizi ni:
Kosekanti (ing. cosecant, kifupi csc) - Kosekanti ya pembe ni sawa na
Sekanti (ing. secant, kifupi sec) - Sekanti ya pembe ni sawa na
Kotangenti (ing. cotangent, kifupi cot) - Kotangenti ya pembe ni sawa na
Angalia mengine kuhusu Trigonometry kwenye miradi mingine ya Wiki: | |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary | |
picha na media kutoka Commons | |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Trigonometria kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Trigonometria, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.