Gamma ni herufi ya tatu katika Alfabeti ya Kigiriki.
Inaandikwa Γ (herufi kubwa ya mwanzo) au γ (herufi ndogo ya kawaida). Zamani ilikuwa pia alama kwa namba 3.
Alfabeti ya Kigiriki | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Herufi za kawaida | |||||||
Α α Alfa | 1 | Ν ν Ni | 50 | ||||
Β β Beta | 2 | Ξ ξ Ksi | 60 | ||||
Γ γ Gamma | 3 | Ο ο Omikron | 70 | ||||
Δ δ Delta | 4 | Π π Pi | 80 | ||||
Ε ε Epsilon | 5 | Ρ ρ Rho | 100 | ||||
Ζ ζ Dzeta | 7 | Σ σ ς Sigma | 200 | ||||
Η η Eta | 8 | Τ τ Tau | 300 | ||||
Θ θ Theta | 9 | Υ υ Ipsilon | 400 | ||||
Ι ι Iota | 10 | Φ φ Phi | 500 | ||||
Κ κ Kappa | 20 | Χ χ Khi | 600 | ||||
Λλ Lambda | 30 | Ψ ψ Psi | 700 | ||||
Μ μ Mi | 40 | Ω ω Omega | 800 | ||||
Herufi za kihistoria1 | |||||||
Digamma | 6 | San | 90 | ||||
Stigma | 6 | Sho | 90 | ||||
Heta | 8 | Koppa | 90 | ||||
Sampi | 900 | ||||||
1 Viungo vya Nje: Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje |
Asili ya gamma ni herufi ya Kifinisia ya gimel (tazama makala ya G). Matamshi yake ni kama G ya Kiswahili.
Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fizikia. Imejulikana hasa kama jina la pembe ya tatu katika pembetatu.
Katika fizikia gamma ni alama kwa fotoni hasa mnururisho mkali aina miali ya gamma.
Katika astronomia inatumiwa kuanza hesabu ya nyota katika kundinyota. Katika mfumo wa Bayer inataja nyota angavu ya tatu katika kundinyota fulani.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Gamma, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.