Tim Berners-Lee (* 18 Juni 1955 mjini London, Uingereza) alianzisha wavuti wa walimwengu (WWW) au intaneti ya dunia zima.
Wavuti ni mfumo unaowezesha watu kutazama habari, picha na kurasa kutoka dunia yote kwenye tarakilishi yao.
Tim Berners-Lee | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 18 Juni 1955 |
Kazi yake | mwanasayansi |
1991 Berners-Lee alikuwa mtaalamu wa kompyuta kwenye CERN (taasisi ya kinyuklia ya Ulaya). Maabara ya CERN ziko pande zote mbili za mpaka wa Uswisi na Ufaransa. Haikuwa rahisi kupata mawasiliano kati ya kompyuta pande zote mbili za mpaka kwa sababu kila nchi ilikuwa na utaratibu wake.
Berners-Lee alitunga lugha ya programu HTML (inayotumiwa leo hii kuandika kila karibu kila ukurasa kwenye toovuti hata wikipedia). Alianzisha pia mpango wa kuweka kompyuta kando kama seva kwa watumiaji wengine. Alitunga mipangoy a kupanusha wavuti kote duniani akasisitiza ya kwamba programu zote ziwe programu huria.
Kwa kazi hizi alikuwa baba wa wavuti.
Leo hii anaishi Marekani akiwa profesa kwenye chuo kikuu cha MIT mjini Boston.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tim Berners-Lee kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Tim Berners-Lee, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.