Patrice Evra: Mchezaji mpira wa Ufaransa

Patrice Latyr Evra (amezaliwa 15 Mei 1981) ni mchezaji wa mpira kutoka nchi ya Ufaransa, ambaye anaisakatia kabumbu timu ya Uingereza ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa.

Yeye ni mlinzi wa kushoto ambaye anaweza pia kucheza upande wa kushoto wa uwanja.

Patrice Evra
Patrice Evra: Wasifu, Maisha ya Kibinafsi, Takwimu ya Wasifu
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa {{{tareheyakuzaliwa}}}
Mahala pa kuzaliwa    {{{nchialiozaliwa}}}

* Magoli alioshinda

Mwana wa mwanadiplomasia, Evra alizaliwa mjini Dakar, Senegal, na aliwasili Ulaya kupitia Brussels kutoka Senegal wakati alikuwa na umri wa miaka sita. Yeye alilelewa Les Ulis, Essonne, Ufaransa, ambako aliishi na familia yake kuanzia mwaka wa 1984 hadi 1998 kabla ya kuchukua nafasi yake ya kwanza ya kucheza kandanda ambayo ilimpelek Marsala, Sicily, Italia.

Wasifu

Wasifu wa Klabu

Wasifu wa Mapema

Katika miaka ya yake ya ujana, Evra alianza kazi yake kama winga wa timu ya vijana ya Paris Saint-Germain. Ingawa hakupokea kamwe mkataba wa kitaalima, alichunguzwa na skauti wa timu ndogo ya Italia iitwayo Marsala,ambayo hatimaye walimpa mkataba. Baada ya kucheza mechi 27 msimu wake wa kwanza kama wing'a wa kushambulia, Evra alifunga mabao sita. Msimu ulifuatao, aliichezea timu ya Monza katika Serie B (ligi ya daraja ya pili, Italia), lakini alicheza mechi tatu pekee yake.

Nice

Evra alirudi Ufaransa kuichezea Nice ya Ligue 2, yaani daraja ya pili. Katika mechi zake kadhaa za kwanza, yeye alicheza kama mshambulizi wa mbele. Kutokana na majeraha ya wachezaji wenzake katika klabu hiyo, alifanywa kucheza kama mlinzi wa kushoto wakati wa mchezo wao dhidi ya Stade Lavallois. Katika mechi kadhaa zilizofuata, meneja Sandro Salvioni alimtumia Evra katika safu ya ulinzi. Wakati uliosalia katika msimu huo, Salvioni aliendelea kumbadilisha kati ya nafasi hizo mbili. Evra aling'ara ulinzini baada ya kutajwa kama mlinzi bora wa kushoto katika Ligue 2.

AS Monaco

AS Monaco, ambao walifurahishwa sana na juhudi za Evra ulinzini, walimsaini kutoka Nice kwa ada ambayo haikufumbuliwa kupitia meneja Didier Deschamps. Kwa haraka akawa mchezaji wa kawaida wa ulinzi pamoja na Sebastien Squillaci, Gael Givet, na Julien Rodriguez. Katika msimu wake wa kwanza na klabu hiyo, Monaco ilifika fainali ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) mwaka wa 2004 lakini walishindwa 3-0 na Porto, mchezo ambao Evra alicheza dakika 90. Mchezo wake ulimsababisha kuitwa katika timu ya kitaifa ya Ufaransa.

Mwaka wa 2005, Evra alitajwa nahodha mara kadha. Monaco walipambana msimu huo kwani walichujwa katika raundi za kuhitimu za Kombe la Mabingwa barani Ulaya ya mwaka wa 2005-2006 na mara nyingi msimu huo walikuwa nusu ya meza ya ligi hiyo.

Manchester United

Patrice Evra: Wasifu, Maisha ya Kibinafsi, Takwimu ya Wasifu 
Evra huja mbali lami baada ya mechi dhidi ya Arsenal

Evra alisaini mkataba wa Manchester United tarehe 10 Januari 2006, ada ya uhamisho ikizungukia paundi milioni 5.5 kutoka AS Monaco. Muda wa mkataba huu ulikuwa wa miaka tatu unusu. Kuwasili kwa Evra kuliashiria azma au nia ya Alex Ferguson kutatua shida ya safu la ulinzi ambalo lilikuwa limehangaika tangu Gabriel Heinze alipojeruhiwa. Katika mkutano wake wa kwanza na klabu baada ya kusainiwa, alimuliza nahodha Gary Neville pahali ambapo kanisa karibu ipo.

Aliichezea Manchester United kwa mara ya kwanza siku nne baada ya kusainiwa.Manchester United walishindwa mechi hii ya ligi kuu la Uingereza 3-1 na Manchester City. Mechi yake ya kwanza haikuwa bora kwani alitolewa wakati wa mapumziko ya kwanza yaani hafutaimu. Alicheza mechi yake ya kwanza nyumbani baina ya Liverpool, mechi ambayo Manchester United ilishinda 1-0 jumatano iliyofuata. Awali Evra alikuwa na baadhi ya matatizo ya kujirakibisha na mchezo wa Uingereza, lakini katikati ya msimu wa 2006-07 fomu yake iliboreka sana na alijiimarisha kama mchezaji wa kawaida wa timu ya kwanza. Tarehe 29 Novemba, alifunga bao lake la kwanza la klabu katika mechi ya ligi dhidi ya Everton katika uwanja wa Old Trafford. Baada ya kukaa nje ya kikosi, Evra alirejea tarehe 10 Aprili 2007 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Roma katika uwanja wa Old Trafford. Alichangia Red Devils kuinyuka wageni hao 7-1 bao lake likiwa la mwisho, la kwanza katika ligi hili la Mabingwa. Kutokana na juhudi zake, Evra alichuma mahala katika timu ya mwaka ya PFA.

Katika msimu wa 07-08, Evra akawa mlinzi muhimu katika safu ya ulinzi. Ingawa alicheza mechi 47 katika mashindano yote kwa ujumla, idadi iliyojuu zaidi katika wasifu wake, hakuweza kufunga bao. United ilishinda ligi hiyo kwa mara ya pili mfululizo siku ya mwisho ya ligi. Waliushinda ubingwa huo wakiwa na alama mbili zaidi ya Chelsea. Alicheza mechi kumi katika ligi ya Mabingwa barani Ulaya ya UEFA, pamoja na fainali ambayo United iliichapa Chelsea kwa njia ya penalti mabao 6-5, kufuatia sare ya 1-1 baada ya muda wa ziada. Tarehe 12 Juni, Evra alisaini mkataba wa urefusho wa miaka minne na United, sunobari ambao utamweka Old Trafford hadi mwaka wa 2012.

Evra alicheza mechi 14 za Manchester United za kwanza za msimu wa 2008-09. Hata hivyo, tarehe 5 Desemba 2008, alipigwa marufuku kutocheza mechi nne - iliyofaa kuanza tarehe 22 Desemba 2008 - na alifainiwa paundi 15000 baada ya kupatikana na hatia ya kuwa na tabia isiyo halali na FA. Shtaka hili lilihusishwa na tukio lilotokea baada ya mechi kati ya Chelsea na Manchester United tarehe 26 Aprili 2008. Dafrao lilizuka baina ya wachezaji wa Manchester United wafanyikazi wa Chelsea.

Wasifu wa Kimataifa

Wakati wa Euro 2008, Evra hakujumuishwa kwenya kikosi cha kwanza dhidi ya Romania ndiposa Eric Abidal wa Barcelona apate kucheza. Aliitwa mechi iliyofuata dhidi ya Uholanzi baada ya sare tasa dhidi ya Romania. Ufaransa ilipoteza mechi hiyo 4-1. Mechi ya mwisho katika kundi hicho ilikuwa ni lazima Ufaransa ishinde baina ya Italia. Ufaransa waliopoteza mechi hiyo 2-0 na walibanbuliwa katika mashindano hayo. Baada ya mechi hiyo, kamera ziliwapata Evra na Patrick Vieira wakikaripiana kwenye handaki.

Maisha ya Kibinafsi

Evra amemwoa Sandra ambaye wana mwana mvulana, Lenny. Ana jumla ya ndugu 25, ingawa wawili sasa ni marehemu.

Takwimu ya Wasifu

Klabu Msimu Ligi Kikombe Kikombe cha Carling Europa Zingine Jumla
Matokeo Mabao Matokeo Mabao Matokeo Mabao Matokeo Mabao Matokeo Mabao Matokeo Mabao
Marsala 1998-99 [43] 3 -- -- -- -- -- -- -- [43] 3
Monza 1999-2000 3 0 -- -- -- -- -- -- -- 3 0
Nice 2000-01 5 0 -- -- -- -- -- -- -- -- 5 0
2001-02 34 1 -- -- -- -- -- -- -- -- 34 1
Jumla 39 1 -- -- -- -- -- -- -- -- 39 1
AS Monaco 2002-03 36 2 -- -- -- -- 0 0 -- -- 36 2
2003-04 [46] 0 -- -- -- -- 13 0 -- -- 46 0
2004-05 36 0 -- -- -- -- 9. 0 -- -- 45 0
2005-06 15 0 -- -- -- -- 7 0 -- -- 22 0
Jumla 120 2 -- -- -- -- 29 0 -- -- 149 2
Manchester United 2005-06 11 0 1 0 2 0 0 0 0 0 14 0
2006-07 [43] 1 4 0 1 0 7 1 0 0 36 2
2007-08 [46] 0 4 0 0 0 10 0 1 0 48 0
2008-09 28 0 3 0 2 0 11 0 4 0 48 0
2009-10 14 0 0 0 0 0 4 0 1 0 19 0
Jumla [87] 1 12 0 5 0 32 1 6. 0 165 2
Jumla wa wasifu 296 7 12 0 5 0 [60] 1 6. 0 380 8

Takwimu ni sahihi kutokana na mechi iliyochezwa tarehe 28 Novemba 2009

Tuzo

Klabu

AS Monako

  • Coupe de la Ligue (1): 2003

Manchester United

  • Ligi kuu la Uingereza (3): 2006-07, 2007-08, 2008-09
  • Kikombe cha Carling (2): 2006, 2009
  • FA Community Shield (2): 2007, 2008
  • Ligi kuu ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA) (1): 2008
  • FIFA Club World Cup (1): 2008

Kibinafsi

  • Timu ya mwaka ya ligi kuu ya PFA (2): 2006-07, 2008-09

Marejeleo

Viungo vya nje

Patrice Evra: Wasifu, Maisha ya Kibinafsi, Takwimu ya Wasifu 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

Tags:

Patrice Evra WasifuPatrice Evra Maisha ya KibinafsiPatrice Evra Takwimu ya WasifuPatrice Evra TuzoPatrice Evra MarejeleoPatrice Evra Viungo vya njePatrice Evra15 Mei1981Manchester UnitedTimu ya taifaUfaransa

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

JidaMuda sanifu wa duniaDMagonjwa ya machoViwakilishi vya pekeeVivumishi vya pekeeNyweleWanyamaporiLigi ya Mabingwa AfrikaKiraiUongoziMkoa wa RuvumaHarakati za haki za wanyamaJioniChombo cha usafiriKiambishi tamatiMkutano wa Berlin wa 1885UnyenyekevuSeli za damuMawasilianoChuchu HansMahariFutiSheriaUchumiElementi za kikemiaRamadan (mwezi)Haki za watotoOrodha ya shule nchini TanzaniaBob MarleyTamthiliaLugha ya taifaNyanja za lughaMzeituniMalawiIsaWapareMwakaUbunifuJumaIsraeli ya KaleKiswahiliTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaKiburiMkoa wa RukwaKoloniPasakaMagavanaVivumishi vya urejeshiMnururishoGPapaUundaji wa manenoZuhuraUsawa wa kijinsiaSeliAlama ya barabaraniMitume na Manabii katika UislamuKilimanjaro (Volkeno)SomaliaMamaliaRadiHerufiMtakatifu PauloEngarukaTausiDhahabuMfuko wa Taifa wa Hifadhi ya JamiiFigoUnyevuangaUhifadhi wa fasihi simuliziMkoa wa SongweBilioniKabilaShomari KapombeShengKoala🡆 More