Mnyama Ngozi-Miiba

Nusufaila na ngeli:

Mnyama ngozi-miiba
Shashile katika Kenya (Diadema setosum)
Shashile katika Kenya (Diadema setosum)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Deuterostoma
Faila: Echinodermata
Ngazi za chini

  • †Homalozoa
    • †Homostelea
    • †Homoiostelea
    • †Stylophora
    • †Ctenocystoidea
  • Crinozoa
    • Crinoidea (Mileli-bahari)
    • †Paracrinoidea
    • †Cystoidea
    • †Edrioasteroidea
  • Asterozoa
    • Asteroidea (Viti vya pweza, nyota-bahari)
    • Ophiuroidea (Changa-maji)
  • Echinozoa
    • Echinoidea (Shashile, poe, chani n.k.)
    • Holothuroidea (Kojojo, jongoo la pwani n.k.)
    • †Ophiocistioidea
    • †Helicoplacoidea
    • †?Arkarua
  • †Blastozoa
    • †Blastoidea
    • †Eocrinoidea

Wanyama ngozi-miiba (kutoka Kiholanzi stekelhuidigen) ni wanyama wa bahari ambao wana ngozi yenye miiba na ulinganifu wa pembetano ingawa wahenga wao walikuwa na uwenzipacha. Hata lava wao wana uwenzipacha lakini hukuza pande tano wakiwa wazima. Mifano ya wanyama ngozi-miiba ni viti vya pweza, changa-maji, shashile, chani na kojojo.

Mwili wa wanyama ngozi-miiba una pande tano na umefunikika kwa ngozi yenye fuwele za kalsiti (kabonati ya kalisi) ziitwazo ossicles (vifupa). Kwa hivyo wanyama hawa wana aina ya kiunzi cha nje. Vifupa vya kiunzi hicho vimeunganika kabisa, kama kwa shashile na jamaa, au vimeunga kwa viungo, kama kwa viti vya pweza, changa-maji na kojojo. Katika matukio mengi vifupa hivyo vina michomozo kwa umbo la miiba, sugu au chembe (asili ya jina la faila hii).

Vineli vidogo vichomoza kupitia nyeleo za kiunzi. Kwa wanyama ngozi-miiba wengi hivi vinaweza kutumika kwa kusogea. Kwa wengine, kama mileli-bahari, hutumika kwa kukamata mawindo tu. Miguu hii ya neli (tube feet) inaweza kujishikiza chini au kwenye mawindo kwa njia ya mfyonzo.

Picha

Mnyama Ngozi-Miiba  Makala hii kuhusu "Mnyama Ngozi-miiba" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili stekelhuidige kutoka lugha ya Kiholanzi. Neno (au maneno) la jaribio ni mnyama ngozi-miiba.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Mnyama Ngozi-Miiba  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mnyama Ngozi-miiba kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Historia ya WapareWokovuUkuaji wa binadamuPumuMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaAlama ya uakifishajiMaajabu ya duniaPunyetoUfeministiJinsiaUzazi wa mpangoUkabailaKidoleKamusi za KiswahiliMichezo ya watotoWilaya ya NyamaganaBloguHali ya hewaBustaniVielezi vya namnaHekaya za AbunuwasiKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaBendera ya KenyaApple Inc.Mtandao wa kompyutaViwakilishi vya -a unganifuJoseph Sinde WariobaKatekisimu ya Kanisa KatolikiKakaMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaUkoloniMwanaumeMsamiatiKinjikitile NgwaleIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Kitenzi elekeziMafuta ya petroliMkoa wa MtwaraKiraiUsawa (hisabati)Vita Kuu ya Kwanza ya DuniaUislamuNge (kundinyota)Homa ya manjanoUgonjwa wa kuharaHistoria ya UislamuWanyaturuIntanetiMtoni (Temeke)ChawaBenderaMrisho MpotoLimauHistoria ya ZanzibarFacebookJamhuri ya Watu wa ZanzibarBikira MariaMandhariChristopher MtikilaVipera vya semiMivigha26 ApriliNamba za simu TanzaniaKiharusiMfumo wa upumuajiTulia AcksonRufiji (mto)Soko la watumwaVivumishi vya -a unganifuAzimio la ArushaKapteniBahari ya HindiVivumishi vya kuonesha🡆 More