H.
Kizamiachaza | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kizamiachaza wa Ulaya | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Vizamiachaza ni ndege wa jenasi Haematopus, jenasi pekee ya familia Haematopodidae. Ndege hawa ni weusi au weusi na weupe na wana domo na macho nyekundu na miguu pinki au myeupe. Huonekana pwani kwa kawaida ambapo hutafuta chakula wakiingiza domo lao kwa matope. Hula wanyamakombe, mwata, nyungunyungu na lava wa wadudu, pengine wanyama ngozi-miiba, kaa na samaki pia. Ndege wanaokula wanyamakombe wana domo lenye ncha nyembamba kama ubapa na hulitumia kulifungua kombe ikikata musuli wa mnyama. Wale wanaokula nyungunyungu wana domo kama msharasi. Hii ni kwa sababu ya uchakavu. Vizamiachaza hutaga mayai 2-4 chini ndani ya tundu ya kina kifupi.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kizamiachaza, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.