Mkoa wa Kara ni mojawapo ya mikoa mitano ya Togo.
makao makuu ya mkoa yako mjini Kara.
Mkoa una eneo la kilomita za mraba 11,738. Idadi ya wakazi imekadiriwa kufikia 957,600 kwenye mwaka 2020.
Miji mingine katika eneo la Kara ni pamoja na Bafilo, Bassar, na Niamtougou .
Mkoa wa Kara umegawanywa katika wilaya za Assoli, Bassar, Bimah, Dankpen, Doufelgou, Keran, na Kozah .
Kara iko kaskazini mwa Mkoa wa Kati na kusini mwa Mkoa wa Savanes. Upande wa magharibi iko Ghana, na upande wa mashariki iko Benin .
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mkoa wa Kara, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.