Mkoa wa Savanes ni mojawapo ya mikoa mitano ya Togo.
Iko kwenye kaskazini ya nchi hiyo. Jina la Savanes linamaanisha Savana yaani eneo pakavu penye manyasi na miti kiasi tu.
Mkoa wa Savanes una eneo la kilomita za mraba 8,460. Idadi ya wakazi ilikadiriwa kufikia 1,017,100 kwenye mwaka 2020.
Makao makuu ya mkoa yako mjini Dapaong. Mji mwingine katika mkoa huo ni Mango.
Savanes imegawanywa katika wilaya za Kpendjal, Oti, Tandjouare, na Tone.
Kusini mwa Savanes uko Mkoa wa Kara.
Mipaka mingine ya mkoa huo ni kwa nchi jirani za Ghana (magharibi), Burkina Faso (kaskazini) na Benin (mashariki).
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mkoa wa Savanes, Togo, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.