Milima Ya Lebanoni

Milima ya Lebanoni ni safu ya milima katika nchi ya Lebanoni inayoanza katika Syria.

Inaelekea sambamba na pwani ya Mediteranea na milima ya Lebanoni ndogo. Mwelekeo wa safu ni kutoka kaskazini kwenda kusini kwa urefu wa kilomita 240. Kati yake, kilomita 160 ziko ndani ya Lebanoni na kilomita 80 ndani ya Syria.

Milima Ya Lebanoni
Mwerezi kwenye milima ya Lebanoni.
Milima Ya Lebanoni
Mwerezi kutoka milima ya Lebanoni ni nembo ya kitaifa ya nchi ya Lebanoni.

Upande wa magharibi kuna tambarare nyembamba kando ya pwani ya bahari na upande wa mashariki ni bonde la Beka'a na ng'ambo yake ni safu ya Lebanoni ndogo.

Sehemu ya juu ni mlima Qurnat as Sawda' wenye kimo cha mita 3,088 juu ya UB. Kuanzia mwezi Novemba hadi Aprili milima ya juu hufunikwa na theluji iliyosababisha milima kuitwa "leban" yaani nyeupe.

Zamani palikuwa na misitu minene lakini miti imekatwa tangu nyakati za kale na leo hii ni miti michache iliyobaki. Taarifa nyingi za Biblia zinataja miti ya Lebanoni iliyotumiwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, hekalu la Yerusalemu na pia kwa meli (kwa mfano Kitabu cha kwanza cha Wafalme 5:20 au Ezekieli 27:5). Mti maarufu zaidi wa Lebanoni ni mwerezi.

Milima ilikuwa kimbilio la vikundi vingi vilivyoteswa penginepo, kwa mfano Wakristo Wamaroni, Waislamu Washia na Wadruzi.

Milima Ya Lebanoni Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Lebanoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

KaskaziniKilomitaKusiniLebanoniMediteraneaMilima ya Lebanoni ndogoPwaniSafu ya milimaSyriaUrefu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

ZakaRené DescartesMofolojiaMtakatifu PauloKiambishi awaliBinadamuMamlaka ya Mapato ya TanzaniaBikira MariaKifua kikuuJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaDumaShinaAfrika KusiniAfande SeleInstagramTamathali za semiWaluguruKitenzi kikuuKumaAir TanzaniaBiblia ya KikristoWamasaiViwakilishi vya urejeshiChombo cha usafiriImaniKwaresimaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaKalendaAzimio la kaziTesistosteroniMagonjwa ya kukuMwakaHistoria ya KanisaHistoriaKifo cha YesuSumakuVita Kuu ya Kwanza ya DuniaAngkor WatMillard AyoInshaMkoa wa MwanzaZana za kilimoWanyama wa nyumbaniHekalu la YerusalemuMbuga za Taifa la TanzaniaBrazilChama cha MapinduziJustin BieberAgano JipyaMwenyekitiJakaya KikweteZiwa ViktoriaMbooTarafaUsiku wa PasakaSomo la UchumiMwanzoNgome ya YesuKihusishiMsamiatiAlama ya barabaraniKisaweKupatwa kwa MweziMethaliKhadija KopaAsili ya KiswahiliAsiliSanaa za maoneshoWiki CommonsFani (fasihi)Namba za simu TanzaniaUbongoMaajabu ya duniaMkondo wa umemeTreniClatous ChamaTunu Pinda🡆 More