Theluji (kutoka Kiarabu ثلج, thalj) ni aina ya pekee ya barafu ya maji.
Inapatikana kama usimbishaji unaotelemka kwa maumbile ya barafu ya fuwelia. Fuwele za theluji ni ndogo; muundo wa fuwele unaonekana kwa macho matupu kama fuwele ni kubwa. Vipande vyake ni vyembamba sana, hivyo theluji hutelemka nyepesi si kama vipande vizito vya mvua ya mawe.
Theluji haipatikani kwa halijoto juu ya 0 C°. Katika Afrika inaweza kutokea tu kwenye milima mirefu kama mlima Kilimanjaro na Mlima Kenya.
Theluji hutokea kama mvuke wa maji mawinguni unafikia halijoto chini ya -10 C°. Maji mawinguni yanaweza kukaa kiowevu (majimaji) hata chini ya 0 C° kwa muda. Matone yake madogo sana yanaanza kushikana na punje ndogo za vumbi hewani na kuganda. Fuweli ndogo (chini ya mm 0,1) hutokea. Kadiri zinavyokua na kuwa nzito zinaanza kushuka. Njiani mvuke baridi inashikana na fuweli zinazoendelea kukua. Maumbile yanatokea ya kufanana na picha ya nyota.
Watu katika nchi baridi wamezoea kutofautisha aina mbalimbali za theluji. Lugha nyingi zina maneno ya pekee kwa ajili ya aina tofauti za theluji, kama ni nyepesi au nzito, chepechepe au kavu, mpya au kama imeshakaa muda fulani.
Theluji inatokea:
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Theluji, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.