Mariah Carey: Mwimbaji wa Amerika na mtunzi wa nyimbo (aliyezaliwa 1969)

Mariah Carey (alizaliwa 27 Machi 1969) ni mwanamuziki, mtunzi, mtayarishaji na mwigizaji wa Marekani.

Mariah Carey
Mariah Carey, mnamo Mei 2013
Mariah Carey, mnamo Mei 2013
Maelezo ya awali
Amezaliwa 27 Machi 1969 (1969-03-27) (umri 55)
Aina ya muziki R&B, pop, hip hop, dance
Kazi yake Singer, songwriter, model, record producer, actress
Aina ya sauti Alto
Miaka ya kazi 1988–hadi sasa
Studio Columbia, Virgin, MonarC, Island
Tovuti www.mariahcarey.com

Alitengeneza albamu yake iliyofanya vizuri katika masoko mbalimbali na chati mbalimbali mwaka 1990, chini ya studio ya Columbia Records chini ya Tommy Mottola na kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kufikisha wimbo katika nafasi ya kwanza nchini Marekani. Hii ikiwa ni chati ya Billboard Hot 100. Baada ya kuolewa na Mttola mwaka 1993, mfululizo wa nyimbo bora zilimfanya moja kati ya wanamuzki bora wa Columbia na pia alikuwa anaongoza katika mauzo ya albamu mbalimbali. Kwa mujibu wa gazeti la Billboard Carey alikuwa mwanamuzi mwenye mafanikio zaidi katika miaka yab 1990 nchini Marekani

Kufuatia kuachana na Mottola mwaka 1997, Carey alianza kuingiza vionjo vya hip hop katika albamu zake, na kufanikiwa kwa wastani. Umaarufu wake aulianza kuisha baada ya kuondoka Columbia mwaka 2001. Baadae alisaini mkataba na studio ya Virgin Records lakini baadae aliachishwa kutoka katika studio hizo, hii ikiwa ni baada ya kupata matatizo ya akili yaliyotangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, lakini pia ikiwa ni baada ya filamu yake ya Giltter kushindwa kufanya vizuri. Mwaka 2002 Carey alisaini mkataba na studio ya Island Records na baada ya kupata matokeo mabaya katika kipindi cha nyuma, hatimaye alirejea katika chati ya muziki wa pop,. hii ikiwa ni mwaka 2005..

Carey ameuza nakala zaidi ya milioni 175, za albamu na single dunia nzima.. Carey alitajwa kuwa mwanamuziki wa kike anayeongoza katika mauzo kwa mwaka 2000, hii ikiwa ni katika tuzo za World Music Awards.. Kwa mujibu wa Recording Industry Association of America, Akiwa ameuza nakala za albamu zaidi ya milioni 62.5, Carey ndiye mwanamuziki wa kike anayeongoza kwa mauzo nchini Marekani na kushika nafasi ya 16 kwa kuuza nakala nyingi zaidi ulimwenguni. . Pia anatajwa kuwa mwanamuziki wa kike anayeongoza katika mauzo nchini Marekani katika wakati wa. Nielsen SoundScan

Pia Carey aliongoza katika single za wanamuziki wanaoimba peke yao nchini Marekani. kwa mwaka 2008. Carey alishika nafasi ya sita katika chati ya Billboard ya "The Billboard Hot 100 Top All-Time Artists", na kumfanya kushika nafasi ya pili kwa wanamuziki wa kike wenye mafanikio zaidi katika historia ya 'Billboard Kama nyongeza katika mafanikio yake katika masoko mbalimbali, Carey pia amefanikiwa kupata tuzo za Grammy zipatazo tano. Pia anajulikana kwa sauti yake yenye uwezo wa kubadilika katika nyakati tofauti.

Maisha na muziki

Katika utoto na ujana

Carey alizaliwa katika eneo la Huntington, Long Island, katika jiji la New York. Ni mtoto wa tatu na wa mwisho katika familia ya Patricia Carey (née Hickey), ambaye pia likuwa mwanamuziki na Alfred Roy Carey, ambaye ni mhandisi. Mama yake alikuwa mwenye asili ya Ireland na baba yake alikuwa mchanganyiko wa Afro-Venezuelan na Mmarekani mwenye asili ya Afrika; babu yake kwa upande wa baba aliyeitwa, Roberto Nuñez, alibadilisha jina lake na kuwa Carey ili aweze kuishi nchini Venezuela kuliko kuhamia nchini Marekani. Carey alipewa jina lake kutokana na wimbo wa "They Call the Wind Mariah".. Wazazi wa Carey walitalikiana wakati akiwa na umri wa miaka mitatu tu... Akiwa anaishi katika eneo la Huntington, eneo lenye ubaguzi wa hali juu, wakazi wa eneo hili wamewahi kumpa sumu mbwa wa familia hii, na kuwasha moto katika gari lao. . Baada ya kutalikiana kwa wazazi wake, Carey alipoteza mawasiliano ya karibu na baba yake, wakati huohuo mama yake alikuwa akifanya kazi katika sehemu zaidi ya moja ali aweze kutunza watoto wake. Carey alikuwa akikaa katika chumba chake na kufungulia sauti kubwa ya muziki. Carey alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 3, wakati alipokuwa akimwigiza mama yake alipokuwa akifanya mazoezi ya kuimba nyimbo mbalimbali katika lugha ya kilatini..

Carey alihitimu katika shule ya Harborfields High School iliyopo Greenlawn, New York. Akiwa shuleni, amekuwa akishindwa kuhudhuria darasani mara kadhaa kutokana na kuwa mwimbaji katika studio zinazotengeneza muziki wa demo. hii ikapelekea wanafunzi wenzake kumtungia jina la utani la Mirage Carey aliganikiwa kufanya kazi katika kisiwa cha Long,mbapo Kufanya kazi katika kisiwa cha Long, kulimpa Carey nafasi za kufanya kazi na wanamuziki maarufu kama vile Gavin Christopher na Ben Margulies, ambao akiwa nao aliweza kushiriki katika kuandika nyimbo mbalimbali. Baadae alirejea tena katika jiji la New York, ambapo Carey aliweza kufanya kazi na kulipa kodi ya nyumba ikiwa ni pamoja kufanya kazi katika duka la urembo. Hatimaye aliweza kuimba kama mwimbaji wa nyuma katika single ya Puerto Rico ulioimbwa na Brenda K. Starr.

Mwaka 1988, Carey alikutana na Tommy Mottolla wa studio za Columbia Records katika sherehe,ambapo Starr alimpa tepu ya Carey. Mottola baada ya kucheza tepu hiyo, aliipenda. Baadae alimtafuta Carey lakini hakumpata kwani alikuwa ameshalipa. Lakini Mottola alimtafuta Carey na kusaini nae mkataba wa kutengeneza nyimbo na studio hizo. Na huu ndio ukawa mwanzo wa Carey kuingia katika ulimwengu wa muziki.

Mafanikio ya mapema zaidi: 1989–1992

Carey alishiriki katika kuandika nyimbo katika albamu yake ya mwaka 1990 iliyofanya vizuri iliyoitwa Mariah Carey, na emeendela kundika nyimbo nyingi kati ya nyimbo zake mwenyewe. Wakati wa kurekodi, Carey ilionesha kutokuridhishwa na utendaji kazi wa waanadaji wake kama vile Ric Wake na Rhett Lawrence, ambao studio za Columbia ziliwaweka ili waweze kufanya albamu yake kuwa ya kibiashara zaidi .. Baada ya matangazo ya muda mrefu,. hatimaye albamu hii ilifanikiwa kufika katika nafasi ya kwanza katika chati ya albamu mia mbili bora ya Marekani Billboard 200 ambapo ilifanikiwa kukaa katika nafasi hiyo kwa wiki kadhaa.Pia iliweza kufikisha single nne, kutoka katika albamu hii katika nafasi ya kwanza, na kumfanya Carey kuwa maarufu nchini Marekani. Lakini ulipata mafanikio kidogo katika nchi nyingine. Shutuma mbalimbali zilizuka kufuatia kuchaguliwa kwa albamu ya Carey katika tuzo za Grammy, lakini hatimaye Carey alishinda tuzo za Grammy katika Mwanamuziki bora chipukizi, na single iliyofanya vizuri zaidi ya Vision of Love—Best Female Pop Vocal Performance.

Mafanikio ya kimataifa: 1993–1996

Carey na Tommy Mottola walianza mahusiano ya kimapenzi wakati wa kutengeneza albamu yake ya mwaka. 1993. Kenneth Edmonds alishiriki katika kutengeneza albamu hii ambayo baada ya kutoka ndiyo iliyokuwa albamu kutoka kwa Carey yenye mafanikio zaidi ulimwenguni. Albamu hii imekuwa katika chati ya Billboard 200 kwa wiki kadhaa. . It yielded her first UK Singles Chart number-one,

Baadae mwaka 1994, baada ya kutoa wimbo akishirikiana na Luther Vandross wimbo ulioimbwa na Lionel Richie na Diana Rose ulijulikana kama ‘’Endless Love’’ , Carey alitoa wimbo albamu ya ‘’Merry Christmas, Albamu hiyo ilijumuisha nyimbo za kurudiwa kutoka kwa wanamuziki wengine, na albamu hii ilikuwa moja kati ya albamu yake iliyofanya vizuri zaidi nchini Japan Katika miaka iliyofuata, Carey aliibuka kama mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi nchini Marekani hususani katika redio za nchi hiyo. .

Sura na mwonekano mpya:1997–2000

Mariah Carey: Maisha na muziki, Diskografia, Ziara 
Carey katika eneo la Edwards Air Force Base wakati wa kutengeneza ideo ya wimbo wa "I Still Believe" mwaka 1998.

Carey na Mottola waliachana rasmi mwaka 1997. Japokuwa mwonekano wa wawili hawa mbele za watu walikuwa wakionekana kuwa na furaha. Lakini Carey alisema kuwa, Mottola alikuwa akimwendesha sana. Walitangaza kuachana kwao mmwaka 1997, na taratibu za talaka zilikamilika mwaka uliofuatia.Muda mfupi tu baada ya kuachana Carey aliajiri mtayarishaji mwingine wa muziki.

Albamu ya Carey iliyofuatia, Butterfly, ilitoka mwaka 1997, na kufika hadi nafasi ya kwanza katika chati mbalimbali. Ikiwa na single kama vile Honey’’ ikimwonesha Carey akiwa katika hali ya kuvutia zaidi kuliko alivokuwa mwanzo. . Anasema kuwa Butterfly imekuwa mwanzo wa yeye kuweza kujiongoza katika muziki. Mwezi Januari mwaka 2010, Carey alitangaza jina la mvinyo wake utakaokuwa unaitwa Angel Champagne.

Diskografia

    Makala kuu: Mariah Carey discography

Albamu za Studio

Albamu za mjumuisho

  • MTV Unplugged (1992)
  • #1's (1998)
  • Valentines (2000)
  • Greatest Hits (2001)
  • The Remixes (2003)
  • The Ballads (2008)
  • Playlist: The Very Best of Mariah Carey (2010)
  • Angels Advocate (2010)

Ziara

  • Music Box Tour (1993)
  • Daydream World Tour (1996)
  • Butterfly World Tour (1998)
  • Rainbow World Tour (2000)
  • Charmbracelet World Tour (2003–2004)
  • The Adventures of Mimi Tour (2006)
  • Live At The Pearl (2009)
  • Angels' Advocate Tour (2010)

Filamu

Movies
Mwaka Filamu Kazi Tuzo
1999 The Bachelor Ilana
2001 Glitter Billie Frank Golden Raspberry Award for Worst Actress
2002 WiseGirls Raychel
2003 Death of a Dynasty Herself
2005 State Property 2 Dame's Wifey
2008 You Don't Mess with the Zohan Herself
2009 Tennessee Krystal
Precious Mrs. Weiss Breakthrough Performance Award at the Palm Springs International Film Festival
Nominated — Black Reel Award for Best Supporting Actress & Best Ensemble.
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Supporting Actress in a Motion Picture
Nominated — Screen Actors Guild Award for Outstanding Cast in a Motion Picture.
Television
Year Title Role Notes
2002 Ally McBeal Candy Cushnip Episode "Playing with Matches"
2003 The Proud Family Herself Voice

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Mariah Carey: Maisha na muziki, Diskografia, Ziara 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Mariah Carey: Maisha na muziki, Diskografia, Ziara 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

Tags:

Mariah Carey Maisha na muzikiMariah Carey DiskografiaMariah Carey ZiaraMariah Carey FilamuMariah Carey TanbihiMariah Carey MarejeoMariah Carey Viungo vya njeMariah Carey196927 MachiMarekaniMtunziMwanamuzikiMwigizaji

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya Watakatifu wa AfrikaShangaziBiasharaTawahudiDiniKiumbehaiKiarabuMaambukizi nyemeleziSteven KanumbaBarabaraUnyevuangaMaajabu ya duniaKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaLahajaHakiAlgorithimu uchanguajiMaumivu ya kiunoTabataVita Kuu ya Kwanza ya DuniaNafsiNgono zembeMbadili jinsiaArudhiNomino za wingiAfrika ya MasharikiVirusi vya CoronaOrodha ya visiwa vya TanzaniaAzimio la ArushaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaPaul MakondaKiraiKiburiKitenzi kikuuSarataniUjimaMitume na Manabii katika UislamuOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaMgawanyo wa AfrikaKaaKumaHuduma ya kwanzaMahakamaAgano JipyaMtakatifu MarkoAbedi Amani KarumeMagomeni (Dar es Salaam)WimboMandhariWahaInsha ya wasifuIyungaBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiHadithiLigi Kuu Uingereza (EPL)Uwanja wa Taifa (Tanzania)Haki za binadamuVidonge vya majiraUyahudiUtamaduni wa KitanzaniaJohn MagufuliBarua rasmiHekalu la YerusalemuSheriaUfalme wa MuunganoPichaAli KibaAina za ufahamuMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaRose MhandoIntanetiTafsidaIndonesiaAlama ya uakifishajiWabena (Tanzania)Umaskini🡆 More