Ngeli 3, oda 4:
Kinyama-kigoga | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Koloni ta vinyama-kigoga huko De Beldert, karibu na Tiel, Uholanzi | ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
|
Vinyama-kigoga (tafsiri la jina la kisayansi) ni wanyama wadogo wa maji matamu na ya chumvi wa faila Bryozoa. Ni wanyama sahili na karibu wote huishi katika makoloni yanayoshikamanisha kwenye nyuso mbalimbali, kama vile miamba, mawe, mchanga, makombe na miani. Kwa kawaida wana urefu wa takriban mm 0.5 na wana muundo maalum wa kujilisha unaoitwa lofofori (lophophore), "taji" ya minyiri inayotumiwa kwa kujilisha kwa njia ya kuchuja. Spishi nyingi za baharini huishi katika maji ya kitropiki, lakini kadhaa hupatikana katika mifereji ya bahari na maji ya maeneo ya ncha za dunia. Vinyama-kigoga wameainishwa kama spishi za baharini (Stenolaemata), spishi za maji tamu (Phylactolaemata) na spishi za baharini na pengine maji ya chumvi kidogo (Gymnolaemata). Spishi hai 5,869 zinajulikana. Spishi za jenasi moja huishi peke yao, nyingine zote huishi katika makoloni.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kinyama-kigoga, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.