Kinyama-Kidoto

Familia 4:

Kinyama-kidoto
Koloni ya vinyama-kidoto kutoka Merikani (Barentsia laxa)
Koloni ya vinyama-kidoto kutoka Merikani (Barentsia laxa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Lophotrochozoa
Faila: Entoprocta
Nitsche, 1870
Ngazi za chini

  • Barentsiidae Emschermann, 1972
  • Loxokalypodidae Emschermann, 1972
  • Loxosomatidae Hincks, 1880
  • Pedicellinidae Johnston, 1847

Vinyama-kidoto ni wanyama wadogo wa maji wa faila Entoprocta walio na mwili kwa umbo la kidoto kwenye mwisho wa kikonyo kinamo. Wanafanana na kuhusiana na vinyama-kigoga na kwa kawaida huishi kwenye makoloni kama hawa.

Wanyama hawa huwa na ukubwa wa mm 0.1-7 bila kuhesabu kikonyo. Wana "taji" ya minyiri ambayo silio zao husababisha mikondo ya maji inayochota chembe za chakula kuelekea mdomo. Mdomo na mkundu yote miwili huwamo ndani ya "taji", kinyume na vinyama-kigoga (Ectoprocta) ambao wana mkundu nje ya "taji". Takriban spishi zote za vinyama-kidoto huishi katika makoloni ambayo yameunganishwa kwenye uso wa chini kama miamba, makombe, miani au majengo ya chini ya maji. Spishi nyingine huishi peke yao juu ya wanyama wengine wanaokula kwa kusababisha mikondo ya maji, kama vile sifongo-bahari, vinyama-kigoga au anelidi wanaokaa chini. Baadhi ya spishi hizi zinaweza kusonga polepole. Spishi 150 zote hutokea baharini, isipokuwa spishi mbili zinazoishi katika maji tamu.

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Homa ya manjanoWamandinkaNdovuItifakiUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaHafidh AmeirRoho MtakatifuSaida KaroliShinaWallah bin WallahUkabailaUbaleheTesistosteroniMusaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoUfahamuWizara za Serikali ya TanzaniaSaharaUsafi wa mazingiraVipera vya semiRedioNgw'anamalundiKiungo (michezo)Siku tatu kuu za PasakaFasihi simuliziRobin WilliamsBukayo SakaChombo cha usafiri kwenye majiIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)VichekeshoMisimu (lugha)ShengUislamuUlemavuSisimiziMakabila ya IsraeliAbedi Amani KarumePunyetoMwaka wa KanisaMfumo katika sokaKito (madini)JinsiaKilatiniHarmonizeMashuke (kundinyota)Vita vya KageraMaumivu ya kiunoAzimio la ArushaFonolojiaKitabu cha ZaburiTausiUtandawaziOrodha ya Marais wa TanzaniaZuhura YunusPalestinaSayansiKuhani mkuuKitubioRose MhandoAgano JipyaHektariMapafuHijabuHoma ya dengiUkristo barani AfrikaHekaya za AbunuwasiManchester CityDumaKemikaliHoma ya matumboJumamosi kuuHaiku🡆 More