Karata (kutoka jina la Kireno carta ambalo kwa Kilatini lilimaanisha karatasi; kwa Kiingereza cards) ni kadi au kipande cha karatasi yenye namba, alama au picha ikiwa sehemu ya idadi mfululizo za karata.
Hivyo neno linataja pia mchezo ambao huchezwa na watu mbalimbali kwa lengo la kushindana ili kujifurahisha au kama mchezo wa kamari kwa kupata fedha kutoka kwa wenzao.
Karata hupendwa na watu wa jamii mbalimbali duniani. Michezo hii huwa na mashabiki, si kama mashabiki wa mpira wa miguu.
Kuna aina nyingi za karata na za michezo yao. Aina ya karata iliyoenea katika nchi mblimali kutoka Ulaya huwa na kadi 52 zenye mapambo, alama na tarakimu zinazotumika kucheza arubastini, wahedistini, jore, chanisi, mapiku n.k.
Katika utamaduni tofauti, k.mf. Italia, karata ziko 40 au idadi nyingine.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Karata kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Karata, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.