Kalenga

Kalenga ni kata ya Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51201.

Kalenga
Ramani ya 1914 ya Kijerumani inaonyesha Iringa (iliyoundwa kama kituo cha Kijerumani na kuwa mji wa leo) pamoja "Alt-Iringa", inayojulikana leo kama Kalenga. Hii ilikuwa mji mkuu wa Mtemi Mkwawa.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 11,491 . Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,963 waishio humo. Msimbo wa posta ni 51201.

Hadi mwanzo wa ukoloni Kalenga ilitwa pia "Iringa"; baada ya Wajerumani kuanzisha "Iringa Mpya" (Neu-Iringa) mahali pa mji wa leo, waliita mahali asilia "Iringa ya Kale" (Alt-Iringa).

Kalenga-Iringa na historia ya mtemi Mkwawa

Kalenga 
Ramani ya Kalenga - Iringa mnamo mwaka 1897 (mchoro unaonyesha shambulio la vikosi vya Schutztruppe ya Wajerumani)
Kalenga 
Fuvu la kichwa cha Mtemi Mkwawa katika makumbusho ya Kalenga.

Kalenga ilikuwa makao makuu ya Mtemi Mkwawa aliyeongoza upinzani wa Wahehe dhidi ya ukoloni wa Kijerumani katika miaka ya 1891 - 1896.

Huko Kalenga Mkwawa aliwahi kujenga boma imara ya mawe baada ya kujifunza kuhusu uenezi wa Wajerumani kutoka sehemu za pwani. Boma hii liliitwa Lipuli. Ujenzi ulianza mnamo 1887 ukachukua miaka minne. Mji wote ulijulikana kama "Iringa" maana jina hili linataja mahali palipozungukwa na ukuta.Kalenga-Iringa ilikuwa na sehemu mbili zilizotengwa na mto; upande wa kulia wa mto uliitwa "Unguja", upande wa kushoto "Bagamoyo". Mwaka 1891 kila sehemu ilikuwwa na msimamizi wake walioitwa Ngozingozi na Mtemiuma, waliuawa kwenye mapigano wa Lugalo.

Baada ya kushindwa kwa jeshi la Kijerumani la Schutztruppe katika mapigano ya Lugalo mwaka 1891, Wajerumani walirudi kwa nguvu zaidi wakashambulia Lipuli - Kalenga kwenye Oktoba 1894 kwa silaha kali kama mizinga na bombomu.

Mkwawa alifaulu kukimbia wakati wa kutekwa kwa boma akaendesha vita ya msituni hadi kujiua mwaka 1898 alipoona hatari ya kukamatwa ilhali alijeruhiwa vibaya. Inasemekana Wajerumani walikata kichwa chake na kutuma fuvu lake Ujerumani.

Baada ya kushindwa kwa Ujerumani katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, washindi, hasa Uingereza, walisisitiza fuvu lirudishwe: hivyo kuna fungu 246 katika Mkataba wa Versailles linalotaja fuvu la Mkwawa. Wajerumani walidai baadaye kuwa wanashindwa kulikuta, hivyo walichelewa hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati jeshi la Uingereza lilipokuwa na utawala juu ya sehemu ya Ujerumani ya kwamba Waingereza waliteua fuvu moja katika mkusanyiko wa Makumbusho ya Bremen na kulituma Tanganyika kama fuvu la Mkwawa.

Kalenga kuna makumbusho kwa heshima ya Mtemi Mkwawa na fuvu hilo linahifadhiwa humo tangu kurudishwa mwaka 1954.

Tanbihi

Marejeo

Kalenga  Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania Kalenga 

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa


Kalenga  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kalenga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

KataMkoa wa IringaPostikodi TanzaniaTanzaniaWilaya ya Iringa Vijijini

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya vitabu vya BibliaMzabibuTabataVivumishiChama cha MapinduziUhuru wa TanganyikaAndalio la somoBabeliInshaMichelle ObamaMichezo ya watotoUpendoNamba tasaOrodha ya Watakatifu WakristoKigoma-UjijiMkoa wa RukwaShinaMkoa wa MaraHarusiJokate MwegeloOrodha ya programu za simu za WikipediaBikira MariaAsiaUjasiriamaliUfahamuTamthiliaJumapili ya matawiLigi Kuu Tanzania BaraMkwawaManiiOrodha ya miji ya TanzaniaJamhuri ya Watu wa ChinaAsiliGhanaUtenzi wa inkishafiUkwapi na utaoMeliHoma ya manjanoMwaka wa KanisaHomanyongo CUfufuko wa YesuOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoSheriaKidole cha kati cha kandoSamia Suluhu HassanYesuChombo cha usafiri kwenye majiHistoria ya AfrikaMotoMapafuChris Brown (mwimbaji)Ufugaji wa kukuVieleziMarekaniTarakilishiNabii IsayaHadhiraUmaNgonjeraLucky DubeKaramu ya mwishoHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMbooKiarabuRihannaTungo kiraiTmk WanaumeWimboMbogaUenezi wa KiswahiliJohn Raphael BoccoRedioMacky SallKiunzi cha mifupaSabato🡆 More