Ghostface Killah

Dennis Coles (amezaliwa tar.

9 Mei 1970) ni msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ghostface Killah. Huyu ni mmoja kati ya wanaounda kundi zima la Wu-Tang Clan. Baada ya kundi kuambulia mafanikio yake makubwa kwa kutoa albamu yao ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Enter the Wu-Tang (36 Chambers) , huyu bwana naye akaamua kujiendeleza mwenyewe akiwa kama msanii wa kujitegemea na kuweza kupata mafanikio kibao. Ghostface Killah akatoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Ironman, ambayo ilipokewa vyema sana na watathmini wa masuala ya muziki. Akaendeleza kazi yake, na kutengeneza albamu zake zilizojishindia tuzo kemekem. Albamu hizo ni pamoja na Supreme Clientele, Fishscale, na The Big Doe Rehab.

Ghostface Killah
Ghostface Killah
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Dennis Coles
Pia anajulikana kama Tony Starks, Ironman, General Tony Starks, Pretty Toney, The Wallabee Kingpin, GFK, Ghost Deini, Starky Love, P Tone, Sun God, Wally Champ
Amezaliwa 9 Mei 1970 (1970-05-09) (umri 53)
Asili yake Staten Island, New York, Marekani
Aina ya muziki Hip hop
Miaka ya kazi 1991–mpaka sasa
Studio Razor Sharp, Epic, Starks Enterprises, Def Jam
Ame/Wameshirikiana na Wu-Tang Clan, Theodore Unit, MF DOOM, Rakim, Adult Swim
Tovuti Ghostface's official site

Ghostface Killah ni maarufu mno kwa staili yake ya sauti kubwa, kuchana kwa haraka-haraka, na staili yake ya kuimba kama hataki huku akiwa anatia mbwembwe za maneno ya kitaa-kistori fulani ya kujitambua.

Maisha ya awali

Ghostface Killah amezaliwa na kukulia mjini Stapleton kwenye nyumba za miradi huko New York. Kwenye wimbo wake wa kujielezea mwenyewe wa "All That I Got Is You", Ghost anaelezea maisha yake ya utoto. Ana rap akielezea jinsi alivyokua kwenye mjengo wa vyumba vitatu vya kulalia bila baba yake, ambaye alimwacha tangu akiwa na umri wa miaka sita.

Diskografia

    Makala kuu: Diskografia ya Ghostface Killah

Albamu zake

  • Ironman (1996)
  • Supreme Clientele (2000)
  • Bulletproof Wallets (2001)
  • The Pretty Toney Album (2004)
  • 718 (akiwa na Theodore Unit) (2004)
  • Put It On The Line (akiwa na Trife Da God) (2005)
  • Fishscale (2006)
  • More Fish (2006)
  • The Big Doe Rehab (2007)
  • Ghostdini: The Wizard of Poetry in Emerald City (2009)
  • The Wu-Massacre (akiwa na Method Man and Raekwon) (2009)
  • Customer Love (2010)
  • Agitate, Educate, Organize (2011)

Kompilesheni

  • Shaolin's Finest (2003)
  • The Wallabee Champ (2008)
  • GhostDeini The Great (2008)

Marejeo

Viungo vya Nje



Ghostface Killah  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ghostface Killah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Ghostface Killah Maisha ya awaliGhostface Killah DiskografiaGhostface Killah MarejeoGhostface Killah Viungo vya NjeGhostface Killah19709 MeiMarekaniMuziki wa hip hopWu-Tang Clan

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Vielezi vya mahaliSabatoMwaniShukuru KawambwaKiunguliaWaheheMziziJichoKishazi tegemeziMzeituniKiraiMohamed HusseinMkanda wa jeshiUfugajiWikipediaKishazi huruBawasiriSteve MweusiKiumbehaiAmri KumiDhamiraChakulaNdiziVitenzi vishirikishi vikamilifuMisimu (lugha)Vipera vya semiWahadzabeUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiBenjamin MkapaLongitudoLionel MessiNgiriWilaya ya IlalaLugha ya taifaMuhimbiliMfuko wa Mawasiliano kwa WoteTetekuwangaKiazi cha kizunguUtoaji mimbaOrodha ya kampuni za TanzaniaAlizetiMagharibiTarafaPasakaSah'lomonVivumishiNafsiBiblia ya KikristoTafakuriBendera ya TanzaniaRaiaApril JacksonNyaniMobutu Sese SekoMkunduHurafaKamusi za KiswahiliWilaya ya Nzega VijijiniBikiraTanganyikaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaFasihi simuliziKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniMimba za utotoniFalsafaStadi za maishaJacob StephenPijiniAzimio la ArushaRuge MutahabaDawati🡆 More