Brandi

Brandi (kutoka Kiingereza: brandy) ni kinywaji cha alikoholi kilichotengenezwa kutokana na zabibu au pia matunda mengine.

Brandi
Bilauri ya Brandi

Rangi na ukali

Kuna aina nyingi, kwa kawaida huuzwa ikiwa na viwango vya alikoholi kati ya asilimia 35- 60.

Rangi yake ni kama maji au kahawia. Asili yake ni kukeneka kwa divai au juisi ya matunda iliyochachuka.

Pale inapotoka kwenye chombo cha kukeneka haina rangi sawa na maji. Lakini aina mbalimbali huiva katika mapipa ya mbao na hapo rangi hubadilika kuwa ya kikahawia.

Brandi ya divai

Kufuatana na sheria za Umoja wa Ulaya "brandy" inapaswa kutengenezwa kutoka divai pekee ikiiva baadaye katika mapipa ya mbao. Inaruhusiwa kuongeza sukari. Aina mashuhuri za brandi za divai ni kama vile Cognac (tamka kon-yak, ni asili ya jina la Kiswahili konyagi) na Armagnac kutoka Ufaransa, Brandy de Jerez kutoka Hispania.

Nchi zote zinazotengeneza divai zinajua pia brandi zinazopatikana kwa kutumia maganda ya zabibu yaliyoondolewa juisi tayari ilhali mabaki bado yapo; mabaki hayo huongezewa maji na kuchachua, matokeo hukenekwa. Grappa ya Italia hupatikana kwa njia hiyo.

Katika nchi za Mashariki ya kati brandi ya divai au maganda ya divai huongezewa ladha hasa kwa kutumia mbegu za pimpinella anisum (aniseed) na hii inaleta Ouzo ya Ugiriki, Raki ya Uturuki na Arrak ya Waarabu.

Brandi ya matunda

Kimsingi inawezekana kutumia matunda yoyote kwa brandi ya matunda kwa ukenekaji wa brandi, ama kwa kutoa juisi au kusaga tunda lote halafu kuichachua, kama kiwango cha sukari ndani ya tunda kinatosha.

Watumiaji hupenda ladhaa maalum inayotokana na kila tunda.

Marejeo

Brandi  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Brandi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Brandi Rangi na ukaliBrandi ya divaiBrandi ya matundaBrandi MarejeoBrandiAlikoholiKiingerezaKinywajiMatundaZabibu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Historia ya UrusiRushwaLafudhiKitenzi kikuuSerikaliMikoa ya TanzaniaAli KibaUjimaAngkor WatMvuaDamuViwakilishiKitenzi kishirikishiMkoa wa DodomaMrisho NgassaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaNandyAthari za muda mrefu za pombeJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoBinamuSumbawanga (mji)Benjamin MkapaEe Mungu Nguvu YetuKunguniMariooZana za kilimoMwanamkeTakwimuZakaNahauHistoria ya TanzaniaHarakati za haki za wanyamaKito (madini)SensaKoalaNgome ya YesuJinaBikira MariaKamusi ya Kiswahili sanifuMasharikiThrombosi ya kina cha mishipaMichezoNguvuOrodha ya Marais wa TanzaniaMjiKusiniInjili ya LukaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniFutiDemokrasiaZama za MaweMaradhi ya zinaaMethaliNdiziMjasiriamaliTaasisi ya Taaluma za KiswahiliMkoa wa ShinyangaUmaskiniMsengeSarufiKamusi ya Kiswahili - KiingerezaYesuWikipedia ya KirusiMalawiDubai (mji)Lionel MessiChuraWamasaiUfaransaWapareMkoa wa Unguja Mjini MagharibiSimbaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaLugha ya taifaMfupaMunguIsimu🡆 More