Zen

Zen ni jina la aina ya Ubuddha inayopatikana hasa nchini Japan na katika karne ya 20 imesambazwa katika nchi nyingi duniani.

Ilianzishwa wakati wa karne ya 5 BK katika mkondo wa Ubuddha wa Mahayana nchini China ikaendelea ukua hasa Japan.

Zen
Ensō au alama ya duara ni nembo l Zen: inafundisha ukamilifu lakii pia tupu, hali pasipo na kitu als visuelles Symbol für Zen verwendet
Zen
Zoezi la Zazen wakati wa taamuli

Mkazo wa Zen si mafundisho wala imani bali mazoezi hasa katika hali ya mazingatio kimya kwa lengo la kufikia hali ya mwangaza wa ndani.

Shairi ya kale inaonyesha mwelekeo wa Zen, na hasahasa mstari wa nne::

Mapokeo maalumu nje ya maandiko
bila kutegemea neno wala herufi
moja kwa moja kuonyesha moyo wa binadamu
kuona nafsi ya mwenyewe na kuwa Buddha

Jambo muhimu ni uhusiano kati ya mwalimu na mwanafunzi. Mwalimu ni mtu aliyeona mwangaza akikubali wajibu wa kuwafungulia wengine njia hii pia.

Kufuata njia ya mwangaza ni kazi ya Zazen. Zazen inamaanisha kuketi katika hali ya mazingatio kimya. Mwenyekutafuta mazingatio kimya anaketi chini, mguu mmoja juu ya mwingine. Uti wa mgongo haunyoki na mikono inakaa moja juu ya mwingine bila kuisukuma, ncha za vidole gumba hugusana kidogo. Macho yako wazi kiasi kwa kuangalia chini lakini bila kutazama kitu.

Roho inatazama hali ya wakati bila kutafakai kitu. Mwenye kufuata mazingatio kimya anaangalia pumzi yake na mwili wake, anatazama nafsi yake na fikra. Kwa njia hii anatarajia kuwa kimya kabisa na kufikia hali ya amani ya ndani.


Kurasa husika

Marejeo

Tags:

ChinaJapanUbuddha

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaNovatus DismasMfumo wa lughaVatikaniUtafitiInjili ya MathayoWajitaKipindupinduDhambiKodi (ushuru)NishatiNahauMapenziVivumishi vya idadiViwakilishi vya -a unganifuKifo cha YesuWema SepetuNomino za pekeeMkoa wa MtwaraInstagramKiburiHistoria ya uandishi wa QuraniMfupaChuchu HansUtalii nchini KenyaUaKichomi (diwani)Insha ya wasifuWangoniMethaliUkabailaMotoNomino za wingiKiwakilishi nafsiBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiOrodha ya miji ya TanzaniaUbongoAurora, ColoradoKomaLigi Kuu Tanzania BaraNyokaKuraniMkoa wa Dar es SalaamAina za manenoMfumo wa mzunguko wa damuBiasharaSaratani ya mlango wa kizaziNyangumiEngarukaBustani ya EdeniMtandao wa kompyutaHedhiKiambishi tamatiMagonjwa ya kukuAfrika ya Mashariki ya KijerumaniKengeMtakatifu PauloKamusi ya Kiswahili - KiingerezaMkoa wa IringaMungu ibariki AfrikaElimuParisKiboko (mnyama)Hali maadaAgano JipyaArusha (mji)Chombo cha usafiri kwenye majiMofimuKitenzi kikuu kisaidiziJohn Raphael BoccoKamusi za KiswahiliGesi asiliaVivumishiMivighaKipandausoMichael JacksonHarakati za haki za wanyama🡆 More