Worldcat

WorldCat ni jina la hazinadata kubwa zaidi duniani kuhusu vitabu vinavyopatikana katika maktaba elfu kadhaa kote duniani.

Jina

WorldCat ni kifupi cha "world catalogue" yaani orodha (ya vitabu) ya kimataifa.

Historia

Ilianzishwa mwaka 1967 wakati maktaba za jimbo la Ohio, Marekani ziliungana kuunda taasisi ya "Ohio Computer Library Center" (OCLC) kwa shabaha ya kupeana habari za vitabu vilivyopatikana katika maktaba za vyuo 54 vya Ohio.

Tangu mwaka 1978 maktaba za majimbo mengine ya Marekani yalikubaliwa na jina kubadilishwa kuwa "Online Computer Library Center".

Tangu mwaka 2002 kila maktaba duniani inaweza kujiunga na OCLC. Mwaka 2019 kulikuwa na maktaba wanachama 17,983 katika nchi 123 tofauti.

Huduma

Ukitafuta kitabu kwenye WorldCat itakupa majina ya maktaba wanachama ambamo kitabu hicho kinapatikana. Kama hakuna maktaba iliyo karibu yenye kitabu hicho unaweza kuazima kitabu (karatasi au online) kama maktaba yako ni mwanachama ya WolrdCat na kukubali kuazima kutoka maktaba nyingine.

WolrdCat inatoa pia nafasi ya kupata habari zinazohitajika kwa dondoo kwa kubofya "Cite/Export" (copy a citation).

Maktaba wanachama katika Afrika ya Mashariki

Kenya

(zote ziko Nairobi kama mahali pengine hapatajwi)

  • Kenya Education Management Institute
  • Kenya Institute of Education
  • Kenya Institute of Management
  • Kenya Institute of Management, The
  • Kenya Maritime Authority , Mombasa
  • Kenya Methodist University
  • Herufi House
  • Kenya National Library Services - Buruburu
  • Kenya Power & Lighting Co
  • Kenya School of Law

Tanzania

(zote ziko Dar es Salaam kama mahali pengine hapatajwi)

  • Family History Center,
  • University of Dar Es Salaam
  • African Court on Human and Peoples' Rights
  • Bank of Tanzania Training Institute Library
  • Hamilton Tutorial College
  • ILO Office In Dar es Salaam
  • Main Library; The Eastern Africa Statistical Training Centre
  • Millenium Academy, Nyamagana Mwanza
  • Muhimbili University of Health and Allied Sciences
  • National Institute for Medical Research

Uganda

(zote ziko Kampala kama mahali pengine hapatajwi)

  • Uganda Bible Institute, Mbarara
  • Uganda Christian University, Mukono
  • Uganda Management Institute
  • Uganda Martyrs University
  • Jinja Uganda Family History Center, Jinja
  • Kampala Uganda Family History Center
  • Ministry of Finance, Planning and Economic Development Resource Centre
  • National Library of Uganda

Tanbihi

Marejeo ya Nje

Tags:

Worldcat JinaWorldcat HistoriaWorldcat HudumaWorldcat Maktaba wanachama katika Afrika ya Mashariki[2]Worldcat TanbihiWorldcat Marejeo ya NjeWorldcatDunianiElfuHazinadataJinaMaktabaVitabu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

TafsiriUhuru wa TanganyikaHistoriaMagharibiPijini na krioliJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaWilaya ya UbungoBongo FlavaMandhariMuhimbiliSilabiShinikizo la juu la damuMalariaMoses KulolaWahaVisakaleOrodha ya Marais wa TanzaniaUshairiMkoa wa MwanzaJava (lugha ya programu)Biblia ya KikristoJose ChameleoneOrodha ya mito nchini TanzaniaBahari ya HindiSwalaWaheheAzimio la ArushaTarbiaVichekeshoMohamed HusseinVitenzi vishiriki vipungufuMtume PetroMarekaniLughaNgiriAlizetiFasihiKipazasautiMaudhuiKiambishi awaliMnururishoRedioRohoNdoaRushwaMkoa wa KilimanjaroAfrika KusiniOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaUturukiUchawiMitume wa YesuShetaniAli Hassan MwinyiUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaMkanda wa jeshiUhakiki wa fasihi simuliziApril JacksonFananiUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaJamhuri ya Watu wa China25 ApriliDiniRitifaaKiraiAfrika Mashariki 1800-1845YesuOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaVivumishiBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiSabatoAgano la KaleUundaji wa manenoMnyoo-matumbo MkubwaOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMawasilianoMatumizi ya LughaTabianchi🡆 More