Wilaya Ya Meatu

Wilaya ya Meatu ni wilaya mojawapo kati ya wilaya sita za Mkoa wa Simiyu, Tanzania, yenye postikodi namba 39400 .

Wilaya Ya Meatu
Mahali pa Meatu (kijani cheusi) katika mkoa wa Shinyanga kabla haujamegwa.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 299,619 . Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 366,941 .

Makao makuu ya wilaya yapo Mwanhunzi.

Eneo lake ni kilomita za mraba 8,835.

Mipaka

Meatu imepakana na Wilaya ya Bariadi upande wa kaskazini, Wilaya za Karatu, Ngorongoro na Mbulu upande wa mashariki, Mkoa wa Singida na Maswa upande wa magharibi na Shinyanga upande wa kusini.

Maeneo ya kuhifadhiwa

Karibu nusu ya wilaya ni maeneo yaliyohifadhiwa ambayo ni

Maeneo mengine ya km2 4,582 ni ardhi ya kilimo na ufugaji.

Hali ya hewa

Eneo la Meatu ni nusu yabisi yaani haipokei mvua nyingi. Kiwango cha mvua kinapungua kutoka kaskazini kuelekea upande wa kusini ambako ni milimita 400 pekee zinazonyesha kwa mwaka ilhali sehemu za kaskazini zinapokea milimita 900. Kiwango cha mvua huweza kuwa tofauti kila mwaka ambayo ni tatizo kwa ajili ya wakulima.

Uchumi

Uchumi kwa jumla ni wa kilimo na ufugaji. Mazao ya chakula ni hasa mahindi na mtama lakini kilimo cha mahindi huwa na matatizo ya mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya kiwango cha mvua. Kwa hiyo kila baada ya miaka mitano kuna uhaba wa chakula. Wanawake hulima mahali pengi viazi vitamu karibu na mito ya muda mahali ambako ipo.

Udongo hasa upande wa kusini una kiwango kikubwa mno cha magadi na hivyo hufai kwa kilimo cha muhogo ambalo ni zao linalovumulia ukame.

Ufugaji ni muhimu katika wilaya na wastani ya ng'ombe ni 12-13 kila kaya lakini kwa tofauti kati ya ng'ombe 0 na 2,00 kwa kaya.

Zao la biahara muhimu zaidi ni pamba. Watu wameanza kujenga vinu vya kuchambulia pamba kwa hiyo soko la pamba limeboreshwa hata kama mwendo huu unaweza kuleta matatizo ya chakula. Meatu ni eneo lenye pamba nyingi katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga.

Utalii ni tawi la uchumi lililoanza kuchipuka kutokana na nafasi ya kuwinda.

Uchimbaji wa vito umeanza hapa na pale kwa kutumia mbinu za kienyeji.

Marejeo

Viungo vya Nje

Tanbihi

Wilaya Ya Meatu  Kata za Wilaya ya Meatu - Mkoa wa Simiyu - Tanzania Wilaya Ya Meatu 

Bukundi | Imalaseko | Isengwa | Itinje | Kabondo | Kimali | Kisesa | Lingeka | Lubiga | Mbugayabanghya | Mbushi | Mwabuma | Mwabusalu | Mwabuzo | Mwakisandu | Mwamalole | Mwamanimba | Mwamanongu | Mwamishali | Mwandoya | Mwangudo | Mwanhuzi | Mwanjolo | Mwanyahina | Mwasengela | Ng'hoboko | Nkoma | Sakasaka | Tindabuligi


Wilaya Ya Meatu  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Simiyu bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Tags:

Wilaya Ya Meatu MipakaWilaya Ya Meatu Maeneo ya kuhifadhiwaWilaya Ya Meatu Hali ya hewaWilaya Ya Meatu UchumiWilaya Ya Meatu MarejeoWilaya Ya Meatu Viungo vya NjeWilaya Ya Meatu TanbihiWilaya Ya MeatuMkoa wa SimiyuNambaPostikodiTanzaniaWilaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Azimio la ArushaPasakaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaVidonge vya majiraMofolojiaVivumishi vya urejeshiVivumishi vya idadiWahaVivumishi vya kuonesha28 MachiOrodha ya Marais wa MarekaniMapafuMimba kuharibikaLenziIniTanganyika African National UnionHistoria ya UislamuNamba za simu TanzaniaAina za udongoDayolojiaTetemeko la ardhiShahawaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniVirusi vya UKIMWIAina za ufahamuKarafuuTeknolojia ya habariHistoria ya KenyaHarmonizeBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiMtaalaMkoa wa KigomaUongoziHadhiraSensaKamusi ya Kiswahili - KiingerezaBarua rasmiReli ya TanganyikaMkoa wa SongweLatitudoMalawiBaruaUjimaBenderaKuchaKata za Mkoa wa Dar es SalaamInjili ya MathayoKiingerezaMazingiraCédric BakambuUlemavuAlomofuUkabailaNgono KavuSamakiSayansiChombo cha usafiri kwenye majiIsaUsultani wa ZanzibarWanyamweziMarie AntoinetteCosta TitchMaajabu ya duniaNominoNathariRohoUajemiKinuHeshimaMajira ya baridiEdward SokoineFani (fasihi)HakiMnururishoKata za Mkoa wa MorogoroUmaskiniPasaka ya KikristoYesu🡆 More