Waniloti ni watu wenye asili ya bonde la mto Nile ambao wanatumia lugha za Kiniloti, kama vile Wajaluo, Wasara, Wamasai, Wakalenjin, Wadinka, Wanuer, Washilluk, Waateker n.k.
Wanajulikana kwa urefu na weusi wao.
Pamoja na kuwa wengi kati ya wakazi wa Sudan Kusini, wanapatikana pia Ethiopia, Uganda, Kenya na Tanzania.
Waserer wa Afrika Magharibi pia wana asili hiyo.
Upande wa dini, siku hizi walio wengi wanafuata Ukristo, wakizidi kuacha Dini asilia za Kiafrika.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Waniloti, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.