Uzuri

Uzuri ni sifa ya nafsi, mnyama, mahali, tendo, wazo, neno, tungo, sauti, picha au kitu chochote kinachopendeza.

Uzuri
Anga katika Atacama Desert. Uzuri wa uasilia umekuwa mara nyingi kichocheo cha usanii wa binadamu.
Faili:Kelly, Grace (Rear Window).jpg
Grace Kelly. Sura ya binadamu inaweza kuwa na uzuri mkubwa.
Uzuri
Pambo la maua, Jin Dynasty (11151234 BK), Shanghai, China.
Uzuri
Dirisha la rangi katika kanisa la Notre Dame de Paris, Ufaransa. Katika sanaa ya Kigothi, nuru ilitazamwa ufunuo wa kwanza wa Mungu.
Uzuri
Kuba la Kanisa kuu la Florence. Kuanzia tapo la Renaissance huko Ulaya, ulinganifu na uwiano wa vipimo vilitazamwa vya msingi katika suala la uzuri.

Kimsingi, kwa wanaomuamini Mungu, ni sifa yake ambayo inajumlisha zile za umoja, ukweli na wema, na kujitokeza katika utakatifu wa watu wake.

Kwa namna mbalimbali uzuri unachunguzwa na falsafa, sosholojia, saikolojia n.k. na kulengwa na binadamu tangu zamani za kale, hasa kwa njia ya sanaa za aina mbalimbali. Tangu mtu yupo, hawezi kuridhika na mahitaji ya mwili tu.

Pengine uzuri unategemea utamaduni, lakini mara nyingi unapendeza watu wote.

Mang'amuzi ya "uzuri" mara nyingi yanatokana na utambuzi wa ulinganifu na uasilia, unaomfanya mtu ajisikie salama na kuridhika.

Hata hivyo, kwa kuwa mara kadhaa ni mang'amuzi ya binafsi, mithali ya Kiingereza inasema, "beauty is in the eye of the beholder" ("uzuri umo jichoni mwa mtazamaji")hata pengine ni suala la urithi.

Tanbihi

Viungo vya nje

Uzuri 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

MnyamaNafsiNenoPichaSautiSifaTungoWazo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Dodoma (mji)Agano la KaleVirusi vya UKIMWIMishipa ya damuMajigamboAbedi Amani KarumeMkoa wa TaboraHaki za watotoMzeituniVasco da GamaMfumo katika sokaMagonjwa ya machoAgano JipyaRufiji (mto)Mahakama ya TanzaniaUandishi wa barua ya simuUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Hekalu la YerusalemuKhadija KopaUfugajiVitamini CRohoNgw'anamalundiNdege (mnyama)Mbaraka MwinsheheWilaya ya IlalaOrodha ya Marais wa UgandaMkoa wa PwaniJava (lugha ya programu)Pemba (kisiwa)Utoaji mimbaBenjamin MkapaWimboVivumishi vya kumilikiMkoa wa ArushaAthari za muda mrefu za pombeKariakooDiamond PlatnumzKiarabuMwanaumeSadakaPasakaDalufnin (kundinyota)Kalenda ya KiislamuHomoniEl NinyoStadi za lughaMilanoMajira ya mvuaMkoa wa RuvumaHaitiPunda miliaSilabiUundaji wa manenoMkoa wa SingidaVieleziSheriaMpira wa miguuDhamiraMsituOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaLahaja za KiswahiliMadawa ya kulevyaUzazi wa mpangoSiasaLiverpoolJacob StephenMmeaUkristo barani AfrikaVivumishi vya urejeshiDhima ya fasihi katika maishaKutoa taka za mwiliMajiMisemoAnwani🡆 More