Sosholojia

Sosholojia ni fani ya sayansi inayochunguza mwenendo wa kijamii, yaani binadamu katika maisha ya jamii: unavyoanza, unayoendelea, unavyojipanga na unavyosababisha miundo.

Sosholojia
Mwanasosholojia Auguste Comte (1798-1857).

Kwa maneno mengine, sosholojia inamsoma mtu katika mahusiano yake: mtu na mtu, mtu na watu (kundi) na hivyo huweza kugundua tabia zake mbalimbali.

Somo hilo linahusiana na masomo mengine, kama vile anthropolojia, historia, saikolojia na uchumi.

Ni mojawapo kati ya sayansi za jamii nayo inatumia mbinu tofauti za kutambua hali halisi, halafu inazichunguza kimpango.

Jina

Jina la fani hii linatokana na Kilatini ("socius" yaani "mwenzi") na Kigiriki ("λογία, logia" yaani "elimu") pamoja.

Aliyeunganisha kwa mara ya kwanza maneno hayo (mwaka 1780) ni mwandishi Mfaransa Emmanuel-Joseph Sieyès (1748–1836), lakini alichoandika kilichelewa kuchapwa. Mwaka 1838 alifanya vilevile Mfaransa mwingine, mwanafalsafa wa sayansi Auguste Comte (1798–1857). Comte used this term to describe a new way of looking at society.

Faida ya fani hii

Kujifunza sosholojia ni kujifunza kuangalia dunia kwa mapana zaidi, yaani kutoka nje ya mipaka ya tafsiri zetu tulizojiwekea kijuujuu. Ni kukubali changamoto ya kuchunguza upya yale yote tunayoyajua kwa maana za kawaida: matokeo ya uchunguzi huo pengine hupingana na kile tulichokidhani mwanzoni na hivyo kutuwezesha kuuona ukweli katika hali mpya.

Sosholojia hutusaidia kuelewa hali halisi ya jamii ili kuchangia urekebishaji au utengenezaji wa sera mpya. Hutusaidia pia kukuza ujuzi wetu wa jamii mbalimbali na wa mahusiano yetu kijamii, yakiwa mazuri au mabaya vilevile. Hutusaidia tena kuelewa jumuia zetu kubwa au ndogo kama watu wanaoishi pamoja wakifuata mila na desturi za aina moja na kuwa na lengo moja. Hutusaidia kuelewa aina mbalimbali za utamaduni ili kurahisisha ushirikiano.

Historia ya sosholojia

Pamoja na kwamba mizizi ya sosholojia inapatikana katika maandishi ya wanafalsafa wa Ugiriki Plato na Aristotle, somo hilo lilipata kujitegemea katika karne ya 19 likakua haraka katika karne ya 20.

Mababa wake ni hasa Auguste Comte (1798-1857) na Herbert Spencer (1820-1903).

Wengineo ni Karl Marx (1818-1883), Emile Durkheim (1858-1917) na Max Weber (1864-1920).

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

    Vyama vya taaluma hii
    Vyanzo vingine
Sosholojia  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sosholojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Sosholojia JinaSosholojia Faida ya fani hiiSosholojia Historia ya sosholojiaSosholojia TanbihiSosholojia MarejeoSosholojia Viungo vya njeSosholojiaBinadamuFaniMiundoSayansi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

DamuMjasiriamaliMkoa wa ManyaraBiasharaInjili ya YohaneAdolf HitlerUNICEFMadawa ya kulevyaBakari Nondo MwamnyetoKiongoziAfrika ya Mashariki ya KijerumaniKisimaKatumaKamusi za KiswahiliAbedi Amani KarumeBabeliSumakuHistoria ya IranPalestinaHadithi za Mtume MuhammadRafikiKichecheMaskiniUKUTASadakaMaradhi ya zinaaVitendawiliDhamiraViwakilishi vya kuulizaEdward SokoineSamakiNdotoMoses KulolaKanga (ndege)HomoniIsraelAustraliaHekalu la YerusalemuKwame NkrumahAfyaInsha ya wasifuMkoa wa RuvumaAnne Kilango MalecelaAmina ChifupaNafsiHerufi za KiarabuUkwapi na utaoDayolojiaUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiFani (fasihi)Jakaya KikweteMawasilianoOrodha ya milima ya TanzaniaVidonge vya majiraHarusiJiniHistoria ya UrusiUkomaEmmanuel MbogoSerikaliAthari za muda mrefu za pombeKidoleNguruweTungo sentensiMishipa ya damuHifadhi ya Mlima KilimanjaroDaudi (Biblia)Vita vya KageraYatimaNomino za wingiViwakilishi vya pekeeViwakilishi vya sifaItifaki🡆 More