Ugali

Ugali ni chakula kinacholiwa na jamii za kiafrika.

Chakula hiki chenye virutubisho vya wanga hutokana na unga wa nafaka (kama mahindi, mtama, uwele) au muhogo.

Ugali
Mama anayesonga ugali

Ugali hutayarishwa kwa njia ifuatayo: kwanza unachemsha maji kwenye sufuria baada ya kuchemka unachanganya unga kidogo na maji ya baridi pembeni, kisha tia mchanganyiko huo kwenye maji ya moto yaliyo jikoni huku ukikoroga. Utatokea mchanganyiko wa unga na maji ambao unaitwa uji, acha uji huo uchemke kwa muda kisha tia unga kiasi kulingana na uji wako huku ukisonga kwa kutumia mwiko. Endelea kusonga mpaka mchanganyiko ushikamane, mchanganyiko huu ndio hutoa ugali.

Kimaeneo kuna aina mbalimbali za ugali kutegemeana na aina za mazao yanayopatikana.

Ugali huweza kuliwa na mboga ya aina yoyote kama vile mboga majani, sukumawiki, samaki na nyama.

Kawaida ugali huliwa kwa mikono mitupu. Tonge la ugali hufinyangwa kwa mkono kisha kuchovya kwenye maziwa au mchuzi wa maharage, samaki, au nyama ya ng'ombe. Ugali, mapishi yake na jinsi unavyoliwa, hufanana kwa kiasi fulani na foufou toka Afrika Magharibi, na polenta toka Italia. Ugali hujulikana kama nshima nchini Zambia au nsima nchini Malawi.

Viungo vya nje


Ugali  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

MahindiMtamaMuhogoNafakaWanga

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Madhara ya kuvuta sigaraJackie ChanBarua pepeMapafuTundaBungeDaudi (Biblia)KukiVasco da GamaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarMaradhi ya zinaaUfahamuMadiniVivumishi vya pekeeMashariki ya KatiMweziOrodha ya miji ya Afrika KusiniOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaNyweleTaswira katika fasihiMbuga za Taifa la TanzaniaInstagramKitovuMwanza (mji)SabatoJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaDawa za mfadhaikoWangoniInshaLugha ya programuMajira ya mvuaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuKisaweBinadamuViwakilishi vya urejeshiHistoria ya WapareHistoria ya WokovuHadithi za Mtume MuhammadRayvannyJay MelodyInsha ya wasifuKilatiniKombe la Dunia la FIFAKiraiMaghaniKupatwa kwa MweziDhima ya fasihi katika maishaDumaFonetikiWaluguruUwanja wa Taifa (Tanzania)Wimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiNamba za simu TanzaniaUandishi wa inshaNgeli za nominoRaiaTungo kiraiUtamaduniMjasiriamaliMbeguIntanetiMtaalaWizara za Serikali ya TanzaniaBiasharaHafidh AmeirMethaliKiunguliaZabibuAli Hassan MwinyiNabii IsayaIdi AminHoma ya mafuaOrodha ya Magavana wa TanganyikaMatamshiMnyama🡆 More