The O.c.

The O.C.

Kipindi hiki, kilichobuniwa na Josh Schwartz, kinahusu maisha ya kundi la vijana na familia zao wanapoishi mtaani Newport Beach kwenye mji wa Orange County, California.

The O.C.
The O.c.
Nembo ya The O.C.
Aina Maigizo ya vijana
Imetungwa na Josh Schwartz
Imeongozwa Dave Bartis (season 1)
Bob DeLaurentis
Doug Liman (season 1)
McG
Stephanie Savage (season 4; co-executive producer seasons 1–3)
Josh Schwartz
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Ina misimu 4
Ina sehemu Orange County, California
Utayarishaji
Sehemu Orange County, California
Muda makisio ni dk. 42
Urushaji wa matangazo
Kituo Fox
Inarushwa na 5 Agosti 2003

The O.C. imeonyeshwa kwenye zaidi ya nchi 50 kote duniani na ilikuwa mojawapo ya vipindi maarufu mnamo 2003. The O.C. ilivutia watazamaji milioni 9.7 katika msimu wake wa kwanza, lakini watazamaji walianza kupungua katika misimu iliyofuatia.

Stesheni zilizoonyesha kipindi hiki

Msimu wa kwanza ulianza saa tatu jioni mnamo 5 Agosti 2003 kwenye stesheni ya Fox nchini Marekani. Pia, ilionyeshwa nchini Canada kwenye stesheni ya CTV.

Nchini Uingereza, kipindi cha kwanza kilianza mnamo 7 Machi 2004 saa tatu usiku kwenye stesheni ya Channel 4.

Nchini New Zealand, kipindi hiki kilionyeshwa kwenye stesheni ya TG4.

Nchini Afrika Kusini, ilianza 1 Aprili 2004 kwenye stesheni ya Go.

Wahusika Wakuu

  • Peter Gallagher aliigiza kama Sandy Cohen, ambaye ni wakili, babake Seth na mumewe Kristen Cohen. Yeye anafungua ofisi yake ya kibinafsi na ni meneja. Mwishowe wa kipindi hiki, anakuwa profesa kwenye chuo cha Berkeley.
  • Kelly Rowan aliigiza kama Kristen Cohen. Yeye ni mkewe Sandy, na mamake Seth. Kabla ya kukutana na Sandy, yeye alipendana na Jimmy Cooper. Amewahi kupata shida ya kulewa.Baadaye, anakuwa mjamzito na mtoto huyo anaitwa Sophie Rose Cohen.
  • Benjamin McKenzie aliigiza kama Ryan Atwood, ambaye ni kijana matata. Mamake alimfukuza nyumbani, na baadaye anachukuliwa na Sandy Cohen kulelewa. Ryan anapendana na Marissa, lakini uhiusiano wao ulipata pandashuka tele. Mwishowe, Ryan na Marissa wanapata ajali barabarani na Marissa anakufa mikononi mwake.
  • Mischa Barton aliigiza kama Marissa Cooper, mpenzi wa Ryan. Yeye ni rafiki wa dhati wa Summer. Yeye pia amepata pandashuka nyingi, kama matumizi yamadawa ya kulevya.
  • Adam Brody aliigiza kama Seth Cohen. Yeye ni mpenzi wa Summer. Baadaye, anamuoa Summer.
  • Rachel Bilson aliigiza kama Summer Roberts, mpenzi wa Seth. Yeye ni mwana wa Dkt. Neil Roberts.

Mafanikio

Msimu Vipindi Saa Mwanzo wa msimu Mwisho wa msimu Mwaka Namba Watazamaji
(milioni)
1 27 Jumanne saa 9:00 jioni (2003)
Jumatano saa 9:00 jioni (2003–04)
5 Agosti 2003 5 Mei 2004 2003–04 #57 9.7
2 24 Alhamisi 8:00 p.m. 4 Novemba 2004 19 Mei 2005 2004–05 #85 7.0
3 25 Alhamisi saa 8:00 jioni (2005)
Alhamisi saa 9:00 jioni (2006)
8 Septemba 2005 18 Mei 2006 2005–06 #105 5.6
4 16 Alhamisi saa 9:00 jioni 2 Novemba 2006 22 Februari 2007 2006–07 #123 4.3

Tuzo

Logie Awards

  • Mnamo 2005, The O.C ilisinda tuzo la Most Popular Overseas Program.

PRISM Awards

  • Mnamo 2006, muigizaji Kelly Rowan alishinda tuzo la Performance in a TV Drama Series Episode.

Teen Choice Award

  • Mnamo 2004, Mischa Barton alishinda tuzo la Choice Breakout TV Star - Female.
  • Mwaka huo huo, Adam Brody pia alishinda tuzo la Choice TV Actor - Drama/Action Adventure.
  • Mwaka wa 2005, Rachel Bilson alishinda tuzo la Choice TV Actress:Drama.

Marejeo

Tags:

The O.c. Stesheni zilizoonyesha kipindi hikiThe O.c. Wahusika WakuuThe O.c. MafanikioThe O.c. TuzoThe O.c. MarejeoThe O.c.CaliforniaNewport Beach

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Simba S.C.Mkoa wa MwanzaWizara ya Mifugo na UvuviVivumishi vya idadiNathariMkoa wa Dar es SalaamKukuKimara (Ubungo)MaadiliDaktariSteven KanumbaUfugaji wa kukuTambikoMoyoMfumo wa JuaStadi za maishaBabeliLongitudoIfakaraPesaMpira wa mkonoLilithLady Jay DeeWayback MachineKiumbehaiAfrikaFigoMziziFani (fasihi)Uhifadhi wa fasihi simuliziOrodha ya makabila ya TanzaniaUkristoMadawa ya kulevyaTume ya Taifa ya UchaguziUkabailaHisiaSayariUjerumaniHistoria ya WapareViwakilishi vya idadiMahakama ya TanzaniaClatous ChamaNimoniaUchumiNileSaida KaroliMuundoVielezi vya namnaWilaya ya UbungoMkoa wa NjombeVisakaleHaitiMwana FAHektariKipazasautiNduniMbeyaZuchuMkoa wa DodomaTendo la ndoaViwakilishi vya kuoneshaWanyaturuKukiMsokoto wa watoto wachangaDar es SalaamSaidi NtibazonkizaOrodha ya majimbo ya MarekaniKabilaVivumishi vya urejeshiAdolf HitlerLeonard MbotelaNgiriBendera ya ZanzibarKisukuruNandy🡆 More