Milima Ya Taurus

Milima ya Taurus (kwa Kituruki Toros Dağları) ni milima ya kusini mwa Uturuki inayotenganisha Bahari ya Mediteranea na mabonde ya Mesopotamia upande wa kusini na nyanda za juu za Anatolia upande wa kaskazini.

Milima Ya Taurus
Hii ni milima ya Taurus.

Safu za milima hii zina urefu wa kilomita 1,500 ikianza karibu na Ziwa Eğirdir kwenye magharibi na kuelekea hadi mpaka wa mashariki wa Uturuki.

Milima ya Taurus hugawanywa katika safu tatu kuu kutoka magharibi hadi mashariki kama ifuatavyo:

  • Taurus ya Magharibi (Batı Toroslar)
    • Akdağlar, Milima ya Bey, Mlima Katrancık, Mlima wa Geyik.
  • Taurus ya Kati (Orta Toroslar)
    • Milima ya Akçalı, Milima ya Bolkar, Milima ya Anti-Taurusi, Milima ya Tahtalı, Mlima Aladaglar.

Jiografia

Katika Taurus ya Kati (milima ya Aladaglar na Bolkar) mawe ya chokaa yamesababisha kutokea kwa maeneo ya karst ambako kiwango cha kawaida cha asidi katika mvua kilisababisha mmomonyoko ya miamba na kuunda baadhi ya mapango makubwa ya Asia.

Mto Manavgat huanzia mteremko wa kusini wa Beydaglari.

Katika historia safu za milima ya Taurus zilikuwa kizuizi kikubwa cha mawasiliano na usafiri kati ya Anatolia yenyewe na pwani ya bahari.

Vivutio

Mbali na kupanda mlima, kuna vituo viwili vya skii katika mlima, moja huko Davras karibu kilomita 25 (16 mi) kutoka miji miwili ya karibu ya Egirdir na Isparta, pili ni Saklıkent kilomita 40 (25 mi) kutoka mji wa Antalya.

Milima Ya Taurus  Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Taurus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

AnatoliaBahari ya MediteraneaKaskaziniKiturukiKusiniMesopotamiaMilimaUturuki

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Chuchu HansSinagogiWMuundo wa inshaUpendoKitufeKuraniRedioBenderaBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiMofolojiaKihusishiAina za udongoSemiDhima ya fasihi katika maishaTungo sentensiJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaAla ya muzikiLugha rasmiAthari za muda mrefu za pombeTabianchiKumamoto, KumamotoHarrison George MwakyembeKombe la Mataifa ya AfrikaPasaka ya KikristoLuis MiquissoneUhakiki wa fasihi simuliziKumaMatumizi ya lugha ya KiswahiliTakwimuViunganishiCédric BakambuKarne ya 20Ugonjwa wa kuharaFarasiMisimu (lugha)KarafuuTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaUchumiVielezi vya mahaliSitiariMethaliTanganyikaSodomaTausiInjili ya YohaneTendo la ndoaUaminifuMavaziStadi za lughaLugha ya kigeniMwanamkeKiunguliaJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoWanyamweziUsikuHistoria ya ZanzibarVitenzi vishirikishi vikamilifuDakuHedhiMsituTupac ShakurNomino za pekeeNgome ya YesuKipajiKabilaMwakaKichochoHuduma ya kwanzaUkooHoma ya mafuaNathariDiplomasiaAfrika Mashariki 1800-1845Herufi za KiarabuJokate MwegeloVita vya Kagera🡆 More