Magimbi

Magimbi, majimbi au nduma (Kiing.

Hupatikana sehemu mbalimbali duniani. Yanafanana na viazi au hata matunguu lakini huitwa mashinagimbi. Mmea wao huitwa mgimbi, mjembe, mjimbi au myugwa (Colocasia esculenta) unaoainishwa katika familia Araceae.

Magimbi
Majani ya magimbi
Magimbi
Magimbi sokoni

Magimbi hupendwa sana na watu, hasa kwenye msimu wa Ramadhani kama futari. Mara nyingi hupikwa kwa nazi. Na watu wa Unguja huita zege kwa sababu tu, chakula kitamu na ukila sana unavimbirwa haraka mno. Isitoshe hakiishi haraka tumboni. Kuna miundo mingi ya upishi wa magimbi, aidha kwa kuchemsha tu (chukuchuku) au utie na nazi (hasa kwa watu wa Pwani), yaani, Tanga, Mombasa, Kilwa, Zanzibar na kwingineko. Chakula hiki hakina tabia ya kuliwa sana katika miezi ya kawaida. Ndiyo maana upatikanaji wake wakati mwingine inakuwa vigumu kiasi. Kuna baadhi ya maneo hupatikana sana, lakini kwingineko inakuwa shida. Mara nyingi yanauzwa masokoni au katika masoko yasiyo rasmi, yaani, barabarani.

Colocasia esculenta inasemekana ina asili ya huko kusini mwa India na Asia ya Kusini, lakini vilevile huko ndiko hasa inakolimwa mno. Barani Afrika, Oceania na India Kusini ni chakula kikuu na huenda ikawa ni miongoni mwa vyakula vilivyowahi kulimwa tangu hapo awali. Vilevile inaaminika ya kwamba chakula hiki ni maarufu huko India, Nepal na Bangladesh, na kutoka huko kinaenea hadi Kusini mwa Asia, Mashariki ya Asia na Visiwa vya Pasifiki; magharibi hadi Misri halafu kusini kisha Mashariki na Magharibi mwa bara la Afrika. Kutoka huko yakaenea hadi huko visiwa vya Karibi na Amerika.

Viungo vya Nje

Tags:

ChakulaDuniaFamilia (biolojia)KiaziKiing.MmeaShinaShinagimbiTunguuw:taro

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mohamed HusseinTafakuriMadiniBikira MariaMbwana SamattaZabibuWagogoRoho MtakatifuMwanamkeKisononoAla ya muzikiMuungano wa Tanganyika na ZanzibarViwakilishi vya kumilikiJokate MwegeloHistoria ya ZanzibarMkoa wa ManyaraHistoriaUbadilishaji msimboMkoa wa KataviMzeituniEl NinyoWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiNyotaVita Kuu ya Kwanza ya DuniaOrodha ya makabila ya TanzaniaMisimu (lugha)Kanisa KatolikiChuo Kikuu cha Dar es Salaam25 ApriliUlumbiArsenal FCMeliWachaggaWameru (Tanzania)MatiniKifaruYoung Africans S.C.UturukiWaheheRamaniSiriMtandao wa kompyutaDivaiOrodha ya nchi za AfrikaNabii EliyaMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaMfumo katika sokaKitenziUsafi wa mazingiraMunguEe Mungu Nguvu YetuMwamba (jiolojia)SerikaliSanaa za maoneshoOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaUpepoNg'ombe (kundinyota)Saidi Salim BakhresaRita wa CasciaHekalu la YerusalemuKipazasautiSimuOrodha ya Marais wa MarekaniMasafa ya mawimbiMbuga za Taifa la TanzaniaGoba (Ubungo)KilimoWaluguruUandishiHistoria ya Wasangu🡆 More