Logi (kwa Kiingereza logarithm) ni namna tofauti ya kuandika namba kipeo (kwa Kiingereza exponent) katika fani ya hisabati.
Kimsingi kazi ya logi ni kujibu swali:
"Idadi gani ya namba fulani tunahitaji kuizidisha ili kufikia namba nyingine?"
Mfano:
Swali: Tunahitaji kuzidisha mara ngapi namba "2" ili tufikie 8?
Jibu: 2 x 2 x 2 = 8; kwa hiyo tunazidisha "2" tatu za kufikia 8.
Kwa hiyo logi ni 3.
Badala ya kuandika kwa kirefu "idadi ya 2 zinazohitaji kuzidishwa ili kupata 8 ni 3"
tunatumia fomula log2(8) = 3
Kwa hiyo hizi mbili ni sawa:
Humo tunatumia namba tatu
Mifano mingine:
Mfano a) log5(625) ni nini?
Swali letu ni: Tunahitaji kuzidisha "5" mara ngapi ili tupate 625?
5 × 5 × 5 × 5 = 625, hivyo tunahitaji 5 nne.
Jibu: log5(625) = 4
Mfano b): log2(64) ni nini?
Swali letu ni: Tunahitaji kuzidisha "2" mara ngapi ili tupate 64?
2 × 2 × 2 × 2 × 2 × 2 = 64, hivyo tunahitaji 2 sita
Jibu: log2(64) = 6
Logi zina uhusiano wa karibu na namba kipeo.
Tukiandika
kitako 2 3 namba kipeo tunamaanisha 23 = 2 × 2 × 2 = 8.
Yaani 2 inatumiwa mara 3 katika kuzidisha ili tupate 8.
Logi inatuambia namba kipeo ni ipi. Katika mfano hapo juu "kitako" ni 2 na "namba kipeo" ni 3.
Hivyo logi inajibu swali: tunahitaji namba kipeo gani kwa namba moja kuwa namba nyingine?
Hapo inaonekana ya kwamba fomula za logi na namba kipeo ni njia mbili za kutaja jambo lilelile, ila tu kwa mtazamo kutoka upande tofauti:
ax = y
log a(y)= x
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Logi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.