Helikopta Ingenuity

Ingenuity (tamka in-ji-nyu-i-ti; kwa Kiingereza lina maana ya ubunifu) ni helikopta ndogo isiyo na rubani (drone) iliyopelekwa kwenye sayari ya Mirihi (Mars) kwenye mwezi wa Februari 2021.

Ilifika pamoja na gari la upelelezi Perseverance kama sehemu ya mradi wa "Mars 2020" wa mamlaka ya anga-nje ya Marekani NASA.

Helikopta Ingenuity
Helikopta ya Mirihi "Ingenuity" baada ya kutolewa kwenye gari la upelelezi

Ingenuity ni helikopta ya majaribio yanayolenga kuonyesha kama chombo cha hewani kinaweza kutumiwa katika upelelezi wa sayari ya Mirihi.

Ingenuity ni kifaa kidogo; vipimo vya bodi yake havizidi sentimita 20, mikono ya rafadha yake (rotor) ina urefu wa mita 1.2 ikisimama juu ya miguu ya sentimita 30. Uzito wake ni kilogramu 1.8 pekee.

Inabeba kamera mbili, moja inayotazama chini yake na moja ya kupiga picha za mazingira. Kuna redio ndogo ya mawasiliano. Haiwezi kuendeshwa kutoka duniani moja kwa moja kwa sababu mawimbi ya redio yanahitaji dakika kadhaa baina ya Mirihi na Dunia, hivyo ina kompyuta ndani yake inayopokea maagizo kutoka duniani na kudhibiti miendo ya helikopta. Kama kila helikopta, inapaa hewani kutokana na mwendo wa rafadha yake, inayofanana na panka iliyofungwa juu ya bodi yake. Ina rafadha mbili zenye mwendo wa kinyume kati yake. Hizo zinaendeshwa na injini ya umeme inayopata nguvu yake kutoka betri. Betri zinachajiwa kwa paneli za sola. Kuna changamoto ya baridi ya usiku kwenye Mirihi. Halijoto hushuka hadi nyuzi 90 chini ya sifuri wakati wa usiku, hali inayoweza kuchosha betri haraka sana.

Changamoto kubwa ni angahewa jepesi la sayari hiyo; kiasi cha hewa kinachopatikana kinalingana na kimo cha kilomita 30 juu ya uso wa ardhi na hadi sasa hakuna helikopta duniani iliyopaa juu ya kilomita 13.

Picha kutoka juu zingesaidia kupanga safari za gari la Perseverance; maana hadi sasa magari kwenye Mirihi yameweza kusafiri polepole sana kwa sababu kila baada ya mwendo wa mita kadhaa, dereva aliye duniani anapaswa kusubiri dakika hadi kupokea picha mpya za eneo lililopo mbele, kuziangalia na kuamua kama ni salama gari liendelee, kutuma maagizo yake kwa kompyuta ya gari na kusubiri tena hadi picha zijazo zimefika. Picha kutoka juu zinaonyesha sehemu kubwa ya eneo litakalopitiwa na hivyo gari lingeweza kwenda mbali zaidi bila kusimama.

Tarehe 19 Aprili 2021 Ingenuity iliruka mara ya kwanza kwa sekunde 39, ikapaa mita 3 hewani na kutua tena.

Ingenuity inatarajiwa kuruka hadi mara tano katika muda wa siku 30 za kwanza ikifika kwenye kimo cha mita 3–5 juu ya uso wa Mirihi kwa sekunde 90 kila safari. Imepangwa kusogea kwa umbali wa mita 50 na kurudi.

Ikiwa ujanja unafanya kazi kama inavyotarajiwa, NASA inaweza kujenga juu ya muundo wake ili kupanua sehemu ya angani ya ujumbe wa Mars wa baadaye. Mradi huo unaongozwa na MiMi Aung huko JPL. Wachangiaji wengine ni pamoja na AeroVironment, Inc., Kituo cha Utafiti cha Ames cha NASA, na Kituo cha Utafiti cha Langley cha NASA.

Ujanja hubeba kitambaa kutoka bawa la Wright Flyer ya 1903, ndege ya Wright Brothers, ndege ya kwanza inayodhibitiwa na wanadamu Duniani, na eneo lake la kuondoka na kutua limepewa jina la uwanja wa Wright Brothers.

Picha

Filamu iliyochukuliwa na kamera ya gari Perseverance inaonyehsa jinsi gani helikopta iliruka mara ya kwanza kwenye Mirihi
Filamu ya katuni inayoonyesha kuruka mara ya kwanza ya ingenuity

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

2021FebruariGariHelikoptaKiingerezaMirihiNASAPerseverance (Mirihi)RubaniSayariUpelelezi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Vivumishi vya pekeeSamia Suluhu HassanHistoria ya IsraelMkoa wa MwanzaBunge la Afrika MasharikiUfaransaShikamooJustin BieberUmaskiniArusha (mji)Mkoa wa Dar es SalaamMnururishoDubaiPasaka ya KikristoDaudi (Biblia)Orodha ya Watakatifu WakristoOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaKitabu cha ZaburiMeena AllyUmoja wa AfrikaBasilika la Mt. PauloWema SepetuUlemavuTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaIsraelKito (madini)Kinembe (anatomia)BaruaKupatwa kwa JuaOrodha ya mikoa ya Tanzania na MaendeleoKondomu ya kikeSilabiMsalabaMamaKalenda ya mweziUmaHifadhi ya mazingiraUenezi wa KiswahiliWilaya ya KilindiJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoHistoria ya uandishi wa QuraniMwanaumeUoto wa Asili (Tanzania)John Raphael BoccoMzeituniNdegeWaheheMotoKamusi ya Kiswahili sanifuMahakama ya TanzaniaUgonjwaMfumo wa upumuajiYoung Africans S.C.KiambishiNeemaDar es SalaamAlasiriKibodiUkatiliMkoa wa TangaNevaUnju bin UnuqKiingerezaMaudhuiOrodha ya nchi kufuatana na wakaziMuhammadWangoniRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMusuliMapambano kati ya Israeli na PalestinaMajira ya baridiWiki CommonsJamhuri ya Watu wa ZanzibarTiktokKrismaLongitudoMfumo katika soka🡆 More