Friedrich Nietzsche

Friedrich Wilhelm Nietzsche (tamka: nits-she; 15 Oktoba 1844 - 25 Agosti 1900) alikuwa mwandishi na mwanafalsafa kutoka Ujerumani.

Friedrich Nietzsche
Friedrich Wilhelm Nietszche

Maisha

Alikuwa mtoto wa mchungaji wa Kiluteri akaendelea kusoma lugha za kale za Kilatini na Kigiriki akawa profesa wa lugha za kale kenye chuo kikuu cha Basel. 1879 alipaswa kujiuzulu kutokana na matataizo ya kiafya na tangu 1889 alionyesha dalili za ugonjwa wa akili akaendelea kutunzwa na mama na dadake hadi kifo chake 1900.

Maandishi

Nietzsche amejulikana kama mwanafalsafa aliyepinga mawazo ya wakati wake na hasa Ukristo. Huhesabiwa kati ya wapizani wa dini kwa ujumla. Akiwa kijana aliathiriwa na mwanafalsafa Schopenhauer pamoja na muziki ya Richard Wagner.

Alipenda sentensi fupi-fupi na sehemu ya kazi zake ni mkusanyiko wa sentensi hizo.

Alitangaza kifo cha Mungu aliyemwona kama dhana ya kibinadamu tu iliyopitishwa na wakati akitabiri ya kwamba kumwaga Mungu kutaleta mvurugu mwingi kwa utamaduni. Badala yake alitangaza kuja kwa "mwanadamu wa juu".

Kati ya vitabu vyake ni:

  • Kuhusu chanzo cha mchezo tanzia (Die Geburt der Tragödie), juu ya Sophokles, Euripides na Sokrates
  • Sayansi ya kufurahia (Die fröhliche Wissenschaft)
  • Akasema Zarathustra (Also sprach Zarathustra)
  • Ng'ambo ya Mema na Mabaya (Jenseits von Gut und Böse)
  • Kisikusiku cha Miungu (Götzen-Dämmerung)
  • Adui wa Kristo(Der Antichrist)
  • Humana, nimium humana (Menschliches, Allzumenschliches)
  • Anguko la Wagner (Der Fall Wagners)
  • Pambazuko (Morgenroethe)

Maneno kadhaa

  • Mungu amekufa! Na sisi tumemwua. Twajifariji namna gani, sisi wauaji? (Gott ist tot! Gott bleibt tot! Und wir haben ihn getötet. Wie trösten wir uns, die Mörder aller Mörder?)
  • Kisichoniua chaniongeza nguvu. (Was mich nicht umbringt, macht mich stärker.)
  • Ukiangalia vilindi kwa muda mrefu vinakuangalia pia. (Wenn du lange in einen Abgrund blickst, blickt der Abgrund auch in dich hinein)
  • Mwanamke alikuwa kosa la pili la Mungu (Das Weib war der zweite Fehlgriff Gottes.)

Tags:

15 Oktoba1844190025 AgostiUjerumani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

DaktariClatous ChamaWahaMwezi (wakati)Cristiano RonaldoRiwayaBahashaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaKina (fasihi)TelevisheniHakiHadithiNomino za jumlaMapinduzi ya ZanzibarNdovuGeorDavieVivumishi vya idadiHoma ya iniUkristoAndalio la somoHerufiAgano la KaleUtoaji mimbaViwakilishi vya kuoneshaKadhiUrenoMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaDamuJohn MagufuliShinikizo la juu la damuWagogoUmoja wa MataifaUchawiInshaMlongeFasihiSakramentiUaBiasharaHussein Ali MwinyiAlama ya uakifishajiEthiopiaWasukumaAzam F.C.NafsiMsikitiMkwawaHistoria ya IsraelWokovuMkunduApple Inc.HeshimaRitifaaWarakaMafumbo (semi)MnyamaTundaVita Kuu ya Kwanza ya DuniaMartin LutherHistoria ya TanzaniaMziziKitenzi kikuuHafidh AmeirHadhiraMnyoo-matumbo MkubwaBustaniAfrika ya MasharikiOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaHifadhi ya mazingiraMikoa ya TanzaniaHistoria ya ZanzibarBenjamin Mkapa🡆 More