Freetown ni mji mkuu pamoja na badari kubwa na kitovu cha uchumi wa nchi Sierra Leone.
Iko kwenye kando la Atlantiki kwenye rasi ya Freetown. Idadi ya wakazi ni 1,070,000.
Jiji la Freetown | |
Nchi | Sierra Leone |
---|
Mji uliundwa 1787 kwa ajili ya watumwa wenye asili ya Afrika waliowekwa huru. Hapo ni asili ya jina "Freetown" linalomaanisha "Mji wa watu huru".
Ulikuwa mji mkuu wa koloni za Uingereza katika Afrika ya Magharibi kati ya 1808 hadi 1874.
Hadi leo Makreoli ambao ni watoto wa watumwa waliopewa uhuru kama walowezi ni tabaka la pekee Freetown wakionekana kwa utamaduni na lugha ya pekee.
Katika miaka ya 1990 mji ulikuwa mahali pa mapigano kati ya wanamgambo na askari za ECOWAS.
Uchumi wa Freetown unategemea hasa bandari. Kuna pia viwanda vya sigara, vya kutengeneza petroli, vya chakula na za kusafisha almasi.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Freetown, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.