Ngeli 2:
Konyeza-vichanio | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Konyeza-vichanio (Bolinopsis mikado) | ||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||
| ||||||
Ngazi za chini | ||||||
|
Konyeza-vichanio (kutoka Kiing. comb jelly) ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa bahari ambao huainishwa katika faila Ctenophora (kutoka Kiyunani κτείς = kichanio, na φέρειν = kubeba). Hawakaziki kamwe lakini huogelea majini kama konyeza wengine. Na kama wanyama-upupu wote mwili wa konyeza-vichanio umeumbwa kwa tabaka la kolajini (collagen) na proteoglycans lililofunikwa na seli nje na ndani, lakini unene wa matabaka haya ya seli ni seli mbili kinyume na matabaka ya wanyama-upupu ambayo yana seli moja tu. Tabaka la nje la seli liitwa epidermi (epiderm) na tabaka la ndani liitwa gasterodermi (gastroderm). Kati ya mwili ni uwazi ulio na kipenyo kikubwa kiasi juu (“mdomo”) na vipenyo vidogo viwili chini (“mikundu”). Kipande cha juu cha uwazi huu ni kama koromeo na mdomo wake unaweza kufungwa. Kipande cha chini ni kama tumbo. Takriban spishi zote zina safu nane za “vichanio” vilivyoumbwa kwa vijisinga vingi ambavyo vinapiga chini ili kusukuma mnyama mbele (asili ya jina lao). Spishi nyingi zina minyiri miwili inayotumika kwa kukamata mawindo kwa msaada wa seli za kunata (colloblasts).
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Konyeza-vichanio, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.