Cordoba (kwa Kihispania: Córdoba, tamka kor-do-ba) ni mji wa kihistoria wa Andalusia kusini mwa Hispania kando ya mto Guadalquivir.
Ni makao makuu ya mkoa wa Cordoba. Kuna wakazi 321,000.
Kwa jina la Corduba ulikuwa mji mkubwa wa Hispania kusini wakati wa Dola la Roma.
Tangu karne ya 3 ulikuwa makao ya askofu. Askofu Ossius wa Corduba alishiriki katika Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325).
Baadaye mji ulikuwa sehemu ya falme za Wavisigothi na Bizanti.
Mwaka 711 ulivamiwa na Waarabu Waislamu ukawa mji mkuu wa utemi na baadaye Ukhalifa wa Wamuawiya wa Cordoba. Wakati wa ukhalifa mji ukaitwa Qurtuba (kwa Kiarabu 'قرطبة') na ulikuwa na wakazi nusu milioni: ulikuwa kati ya miji mikubwa duniani ya karne hiyo. Wakazi walikuwa mchanganyiko wa Wakristo, Waislamu na Wayahudi.
Baada ya mwisho wa ukhalifa wa Cordoba mji ulivamiwa na majirani mbalimbali ukawa chini ya utawala wa Waabadiya wa Sevilla, tangu mwaka 1069 chini ya Wamurabitun kutoka Moroko na Wamuwahidun.
Mwaka 1236 jeshi la Wakristo kutoka Hispania kaskazini likateka mji ukabaki chini ya utawala wao na kuwa sehemu ya Hispania ya Kikristo.
Kati ya majengo ya kihistoria kuna
Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Córdoba, Hispania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Córdoba, Hispania, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.