Sildenafil (huuzwa kwa jina la Viagra kati ya majina mengine) ni dawa inayotumika kutibu tatizo la kusimama kwa uume na shinikizo la damu la mshipa mkubwa mapafuni.
Ufanisi wake katika kutibu tatizo kama hilo kwa wanawake haujathibitishwa kikamilifu ingawa zipo kampuni zinazodai kuwa na dawa hii.
Madhara ya kawaida ya dawa hii yanajumuisha maumivu ya kichwa na kiungulia. Tahadhari inatolewa kwa wale ambao wana ugonjwa wa moyo. Madhara makubwa yanajumuisha kusimama kwa uume kwa muda mrefu, ambapo huweza kusababisha uharibifu wa uume.
Wanasayansi wa kampuni ya Pfizer Andrew Bell, David Brown na Nicholas Terrett awali waligundua sildenafil kama matibabu kwa matatizo mbalimbali ya mishipa ya moyo.
Tangu kuanza kutumika kwake mwaka 1998, sildenafil imekuwa matibabu ya kawaida kwa matatizo ya kusimama kwa uume; washindani wake wakubwa ni dawa za tadalafil (jina la kibiashara Cialis) na vardenafil (Levitra).
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sildenafil kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Sildenafil, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.