Papa Stefano I alikuwa Papa kuanzia tarehe 12 Machi 254 hadi kifodini chake tarehe 2 Agosti 257.
Alitokea Roma, Italia, ingawa aliweza kuwa na asili ya Ugiriki.
Alimfuata Papa Lucius I akafuatwa na Papa Sisto II.
Alifundisha kwamba waliobatizwa na madhehebu yaliyojitenga na Kanisa Katoliki wameungana na Kristo moja kwa moja, hivyo hawahitaji wala hawatakiwi kubatizwa tena, tofauti na walivyodai baadhi ya maaskofu, hasa wa Afrika Kaskazini. Baadaye msimamo wake ulienea kote katika Kanisa la Kilatini.
Inasimuliwa kwamba aliuawa na maaskari wa Kaisari Valerian wakati wa Misa .
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, pengine mfiadini.
Sikukuu yake ni tarehe 2 Agosti .
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Stefano I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Papa Stefano I, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.