Wabenedikto

Shirika la Mtakatifu Benedikto (kwa Kilatini Ordo Sancti Benedicti au, kifupi, O.S.B.), ni utawa wa wamonaki wanaofuata Kanuni ya Mtakatifu Benedikto iliyoandikwa mwaka 534 na kuenea kote Ulaya Magharibi kama namna ya kawaida ya umonaki.

Wabenedikto
Benedikto wa Norcia, Mwanzilishi wa shirika

Historia

Wabenedikto hawakubaki katika monasteri zao, wakishika maisha yao ya sala na kazi, bali walijitosa pia kueneza Injili kwa wasio Wakristo, hasa wamonaki wa kiume.

Maarufu sana ni mchango wao upande wa elimu, hasa katika kuokoa maandishi ya zamani na kuyanakili ili kurithisha utajiri wa ustaarabu wa Kigiriki na wa Kirumi pamoja na mapokeo ya Kikristo.

Wabenedikto walistawi katika Karne za Kati, inavyoonyesha sensa ya monasteri 14,000 zilizohesabiwa kabla ya Mtaguso wa Konstanz (1415), ambazo baadhi yake zilifikia kuwa na wamonaki zaidi ya 900.

Uanzishaji wa mashirika mapya, kama yale ya Wafransisko na Wadominiko, ulipunguza umuhimu wao, bila ya kuwamaliza.

Wabenedikto walilipatia Kanisa Katoliki Mapapa wafuatao:

Muundo wa shirika

Wabenedikto, wakiongozwa na abati kwa wanaume au na abesi kwa wanawake, wanaishi katika monasteri ambazo zinajitegemea kiutawala na kuunda mashirikisho 20 ya kiume.

Takwimu

Mnamo tarehe 31 Januari 2005 monasteri za kiume zilikuwa 349 na wamonaki 7.876, ambao kati yao 4.350 ni makasisi pia.

Wamonaki Wabenedikto wa kike mwishoni mwa mwaka huo walikuwa 4.661 katika monasteri 242, mbali na wale wa marekebisho mbalimbali, na masista wa mashirika ya Kibenedikto.

Viungo vya nje

Wabenedikto  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wabenedikto kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Wabenedikto HistoriaWabenedikto Muundo wa shirikaWabenedikto TakwimuWabenedikto Viungo vya njeWabenedikto534UtawaWamonaki

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uwanja wa Taifa (Tanzania)MlongeAlama ya uakifishajiSeliRamaniLigi Kuu Tanzania BaraKaunti za KenyaNomino za wingiSimuUmoja wa MataifaMaleziMethaliMajira ya baridiNgonjeraBinadamuMnazi (mti)Ziwa ViktoriaHadithi za Mtume MuhammadJamhuri ya Watu wa ZanzibarTwigaMpira wa kikapuBongo FlavaOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaKidole cha kati cha kandoFamiliaMjombaMkoa wa TaboraSentensiMbwana SamattaRohoHistoria ya ZanzibarTambikoVirusi vya UKIMWIMwaka wa KanisaMtume PetroSerikaliMnururishoWaluguruUnyevuangaNg'ombe (kundinyota)KonsonantiUkimwiBabeliAndalio la somoMobutu Sese SekoMwarobainiMkoa wa Dar es SalaamEe Mungu Nguvu YetuBarua pepeUaSikioNomino za jumlaMapinduzi ya ZanzibarBrazilNenoUkristo nchini TanzaniaJiografiaMkoa wa MtwaraMagonjwa ya machoMunguP. FunkRayvannyOrodha ya Marais wa UgandaMapenzi ya jinsia mojaDiamond PlatnumzVipera vya semiDiplomasiaIbadaMadhara ya kuvuta sigaraOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaHifadhi ya SerengetiIntanetiYouTube🡆 More