Mshale (wingi: mishale) ni ala ya vita au silaha ndogo ifananayo na mkuki inayorushwa kwa upinde.
Kwa maelfu ya miaka, watu duniani kote wamewahi kutumia upinde na mishale kwa uwindaji na kwa ajili ya ulinzi.
Ushahidi wa kale kabisa wa mshale wenye kichwa cha jiwe ulipatikana Mapango ya Sibudu nchini Afrika Kusini. . Mshale huo unaaminika kuwa ulitumika miaka 64,000 iliyopita.
Ushahidi wa kale kabisa wa matumizi ya upinde kurusha mshale ni wa miaka 10.000 uliopatikana Bonde la Ahrensburg kaskazini mwa mji wa Hamburg, nchini Ujerumani.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mshale, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.