Monoksidi Kabonia

Monoksidi kabonia (pia: Monoxidi ya kaboni, kwa Kiingereza carbon monoxide) ni kampaundi inayounganisha atomi moja ya oksijeni na atomi moja ya kaboni katika molekuli.

Fomula yake ya kikemia ni CO.

Monoksidi Kabonia
Monoksidi kabonia

Inatokea wakati wa kuchoma kaboni, yaani mata ogania, kama kuna oksijeni kidogo tu; katika mchakato wa kawaida hutokea dioksidi kabonia.

Ni fueli nzuri inaoonyesha miale ya buluu wakati wa kuwaka. Katika hali ya gesi ni sumu kali isiyo na ladha, harufu wala rangi.

Inaweza kusababisha kifo kama moto unawaka katika nyumba au jikoni na watu wanaivuta ndani ya mapafu; inaingia katika damu na kuzuia usafirishaji wa oksijeni katika seli nyekundu za damu.

Monoksidi kabonia ina matumizi mbalimbali ya kiteknolojia, kwa mfano katika uzalishaji wa chuma kutoka mbale kwa sababu inaondoa oksijeni kwenye mbale unaoyeyushwa.

Fomula yake ni

    2C + O2 → 2CO

au kwa kupuliza mvuke wa maji katika makaa ya kuwaka

    C + H2O → CO + H2

Iliwahi kutumiwa kama fueli ya magari kwa kuchoma vipande vya kuni kwa joto duni na gesi iliweza kuchomwa ndani ya injini ya gari.

Viungo vya nje

Tags:

AtomiFomulaKaboniKampaundiKemiaKiingerezaMojaMolekuliOksijeni

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WangoniMagharibiMwanza (mji)Mfuko wa Mawasiliano kwa WoteUchawiNimoniaMapinduzi ya ZanzibarHistoria ya ZanzibarKifaruVichekeshoWabunge wa Tanzania 2020Afrika KusiniMkoa wa MaraDuniaMkoa wa RuvumaBikira MariaHalmashauriUlayaMkutano wa Berlin wa 1885Wayback MachineUfahamuMbezi (Ubungo)TanzaniaJokate MwegeloYanga PrincessKoroshoPalestinaMajiMawasilianoVivumishiHistoria ya KiswahiliMaktabaUhakiki wa fasihi simuliziMkuu wa wilayaHistoria ya UislamuMapambano kati ya Israeli na PalestinaUsafi wa mazingiraWizara za Serikali ya TanzaniaYesuNgamiaNambaTulia AcksonMadawa ya kulevyaMbuga za Taifa la TanzaniaRupie ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani25 ApriliStadi za maishaSamia Suluhu HassanShambaKiimboKiswahiliNetiboliKichecheVielezi vya namnaSayansi ya jamiiMoscowArsenal FCBongo FlavaKilimoMsitu wa AmazonMbeya (mji)Fasihi andishiVitenzi vishirikishi vikamilifuSaidi Salim BakhresaMkoa wa KilimanjaroSexShikamooApril JacksonChakulaIsrael🡆 More