Mesrop

Mesrop Mashtots (pia Mesrob Mashtotz, kwa Kiarmenia Մեսրոպ Մաշտոց; Hatsik, Armenia ya Kale, leo nchini Uturuki, 361 hivi - Wagharshapat, Armenia, 17 Februari 440) alikuwa mmonaki, mwanateolojia, mshairi na mtaalamu wa lugha mwanafunzi wa Patriarki Nerses I.

Mesrop
Mesrop Mashtots alivyochorwa mwaka 1776.
Mesrop
Mesrop Mashtots alivyochorwa na Francesco Maggiotto (1750-1805).
Mesrop
Monasteri ya Amaras huko Nagorno Karabakh ambapo Mesrop Mashtots alianzisha shule ya kwanza iliyotumia alfabeti yake.

Anaitwa "Mwalimu wa Armenia" kwa kuwa ndiye aliyebuni alfabeti ya Kiarmenia (406) ili waamini waweze kujua Biblia ya Kikristo akaitafsiri yote akaanzisha shule nyingi akiweka hivyo misingi ya taifa hilo na ustaarabu wake uliolidumisha hata leo kati ya matatizo makubwa ya historia yake, hasa dhuluma za kidini.

Baada ya kufanya kazi ikulu, alipata daraja takatifu na kujiunga na umonaki akaanzisha mtindo wa monasteri kuwa na shule karibu nayo ili kuandaa watu watakaoendeleza elimu ya dini hasa kwa kutafsiri na kunakili vitabu.

Mapema monasteri kubwa zikawa pia na seminari kuu au vyuo vikuu vya teolojia.

Hivyo umonaki wa Armenia ulidumisha utamaduni wa taifa hilo, ambalo lilikuwa la kwanza kupokea Ukristo jumla pamoja na mfalme wake (300) halafu likaushika moja kwa moja hata lilipopitia vipindi vigumu sana.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Filamu

  • Mashtots (1988), directed by Levon Mkrtchyan

Viungo vya nje

Mesrop  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Tags:

Mesrop Tazama piaMesrop TanbihiMesrop MarejeoMesrop FilamuMesrop Viungo vya njeMesrop17 Februari361440ArmeniaArmenia ya KaleKiarmeniaLughaMmonakiMtaalamuMwanafunziMwanateolojiaPatriarkiUshairiUturuki

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Wilaya ya KinondoniMimba kuharibikaTaswira katika fasihiTafsiriUlimwenguLahajaKoroshoDini asilia za KiafrikaWanyaturuChuo Kikuu cha Dar es SalaamUgandaUmoja wa MataifaMwakaMkuu wa wilayaMkoa wa RukwaLeonard MbotelaVichekeshoLatitudo25 ApriliMtaalaOrodha ya milima mirefu dunianiEdward SokoineDhima ya fasihi katika maishaMahakamaOrodha ya miji ya TanzaniaAsidiMivighaLiverpoolHistoria ya IranMuhammadVidonge vya majiraMaandishiUkatiliNyegeVidonda vya tumboAfrika KusiniUtoaji mimbaUajemiSemiSkeliMauaji ya kimbari ya RwandaLady Jay DeeMahakama ya TanzaniaVitamini CUchawiSoko la watumwaRisalaMkoa wa DodomaMaghaniTanganyika (ziwa)TambikoKamusiWaluguruSayariNguruweBenderaMichael JacksonOrodha ya Marais wa UgandaNyotaUkristo barani AfrikaKilimoKhadija KopaMkoa wa ManyaraKiongoziVirusi vya UKIMWINyangumiUgonjwa wa kuharaUundaji wa manenoUenezi wa KiswahiliMziziMfumo katika soka🡆 More